JERRY ft VUMBE - PLANET
Saturday, September 15, 2012
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Ndugu wananchi,
Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi Tanzania Bara utafanyika tarehe 19 na 20 Septemba, 2012. Jumla ya wanafunzi 894,881 wamesajiliwa kufanya mtihani huo ambapo wavulana ni 426,285 sawa na asilimia 47.64 na wasichana ni 468,596 sawa na asilimia 52.36. Aidha, kati ya wanafunzi hao, wapo wanafunzi 874,379 watakaofanya mtihani huo kwa lugha ya Kiswahili na wanafunzi 20,502 watafanya kwa lugha ya Kiingereza ambayo ndiyo waliyoitumia kujifunzia. Wanafunzi wasioona waliosajiliwa kufanya mtihani ni 92 wakiwemo wavulana 53 na wasichana 39. Watahiniwa wenye uono hafifu ambao huhitaji maandishi makubwa ni 495, kati yao wavulana ni 238 na wasichana ni 257.
Mtihani huu utafanyika kwa mara ya kwanza kwa kutumia teknolojia mpya ya ‘Optical Mark Reader’ (OMR), ambapo watahiniwa watatumia fomu maalum za OMR kujibia mtihani na majibu yao yatasahihishwa kwa kutumia kompyuta. Masomo yatakayotahiniwa katika mtihani huo ni Kiswahili, English Language, Sayansi, Hisabati na Maarifa ya Jamii.
Ndugu wananchi,
Maandalizi yote kwa ajili ya mtihani huo yamekamilika ikiwa ni pamoja na kusambazwa kwa karatasi za mitihani, kusambazwa kwa fomu maalum za kujibia mtihani na nyaraka zote zinazohusu mtihani huo. Mafunzo maalum kwa ajili ya matumizi ya fomu za OMR yamefanyika kwa lengo la kuwaandaa watahiniwa, wasimamizi pamoja na viongozi wa elimu katika ngazi mbalimbali ili waweze kutumia ipasavyo teknolojia hiyo.
Ndugu wananchi,
Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi ni muhimu kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla kwa kuwa unahitimisha ngazi ya Elimu ya Msingi na kufungua milango kwa ajili ya elimu ya sekondari. Hivyo, matokeo ya mtihani huu hutumika katika uchaguzi wa wanafunzi wanaojiunga na Elimu ya Sekondari. Kwa kuzingatia umuhimu wa mtihani huo, napenda kutumia fursa hii kutoa wito kwa Maafisa Elimu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha kuwa taratibu zote za mitihani zinazingatiwa ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa mazingira yanakuwa salama na tulivu na kuzuia mianya yote inayoweza kusababisha udanganyifu.
Napenda pia kutoa wito kwa wasimamizi wa mitihani kufanya kazi yao ya kusimamia kwa umakini na uadilifu wa hali ya juu. Wapo baadhi ya wasimamizi ambao wamekuwa wakishiriki katika kuwasaidia watahiniwa kufanya udanganyifu kwenye mitihani. Napenda kuwaasa tena wasimamizi kujiepusha na vitendo hivyo vya udanganyifu kwani serikali haitasita kuchukulia hatua kali za kisheria kwa yeyote atakayebainika kukiuka taratibu za mitihani.
Kwa upande wa wanafunzi watakaofanya mtihani mwaka huu, ninaamini kuwa walimu wamewaandaa vizuri katika kipindi chote cha miaka saba ya Elimu ya Msingi. Hivyo, ni matarajio yangu kuwa mtaufanya mtihani huo kwa utulivu na kuzingatia taratibu zote za mitihani ili matokeo ya mtihani yaoneshe uwezo wenu halisi kulingana na maarifa na ujuzi mliopata katika Elimu ya Msingi. Serikali inawaasa wanafunzi wote kutojihusisha na vitendo vyovyote vya udanganyifu katika mtihani kwani watakaobainika watafutiwa matokeo yao yote ya mtihani.
Ndugu wananchi,
Natoa wito kwa jamii kutoa ushirikiano unaotakiwa katika kuhakikisha kwamba mtihani huo unafanyika kwa amani na utulivu wa kutosha bila usumbufu unaoweza kusababishwa na shughuli za kijamii hasa katika maeneo ya jirani na shule.
Mwisho, napenda kuwaasa tena wanafunzi, walimu na wananchi wote kwa ujumla kujiepusha na vitendo vya udanganyifu wa aina yoyote katika Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi. Nawaomba pia raia wema wasisite kutoa taarifa katika vyombo husika pindi wanapoona au kuhisi mtu au kikundi cha watu kinajihusisha na udanganyifu wa aina yoyote katika mtihani huo.
Nawatakia watahiniwa wote heri na fanaka katika mtihani utakaofanyika tarehe 19 na 20 Septemba, 2012.
MHESHIMIWA PHILIPO AUGUSTINO MULUGO (MB)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
15 SEPTEMBA, 2012
Saturday, September 1, 2012
Friday, August 31, 2012
SULTAN KING ANG'OA JIKO SEPTEMBA 7
Sultan King bwana harusi mtarajiwa
Hamida Maalim akishow love na bwana harusi mtarajiwa Sultan King
Msanii anaefanya vizuri katika game la muziki wa bongo fleva Zanzibar Sultan King anatarajia kufunga ndoa ijumaa ijayo tarehe 7 mwaka huu na party inatarajiwa kufanyika Salama Hall Bwawani.
BIBI BOMBA NAMBA 3 AREJEA ZANZIBAR, AHOJIWA KATIKA NIPE NIKUPE
Mtangazaji wa kipindi cha Nipe nikupe Husna B
Bi Nasra mshindi wa 3 katika shindano la BIBI BOMBA
Bibi Bomba mshindi wa 3 Bi Nasra akihojiwa na Husna B kwenye kipindi cha Nipe Nikupe leo akieleza namna shindano lilivyokuwenda mpaka kupatikana mshindi.
Bi Nasra akishow love na Hamida Maalim mara baada ya kumaliza mahojiano yake.
Mzanzibari aliyeshiriki shindano la Bibi Bomba Bi Nasra linalosimamiwa na Clouds TV na Clouds Fm Jijini Dar es Salaam amerejea Zanzibar akiwa amebahatika kuwa mshindi namba 3 na kujinyakulia kiasi cha shilingi milioni moja na nusu taslim (1,500,000/-)
Bi Nasra maarufu kama Bi Naa alieleza changamoto alizokutana nazo kwa kipindi chote walichokuwa katika nyumba maalum waliokuwa wanaishi na kuibatiza jina la Jumba la Dhahabu kutokana na kukamilika kwa mahitaji yote waliyokuwa wakiyahitaji katika nyumba hiyo.
Alisema walikuwa wakishiriki kwenye michezo na mambo mbalimbali waliohitajika kuyafanya ikiwemo kucheza ngoma, mchezo wa kucheza na Nyoka, kupika na kusuka mikeka.
Katika michezo hiyo ipo michezo ambayo aliweza kushiriki ipasavyo na ipo michezo ambayo hakuweza kushiriki kabisa ikiwa ni kucheza ngoma pamoja na kucheza na nyoka.
Bi Nasra anawashukuru wazanzibari wote na watanzania kiujumla kwa kuweza kumpigia kura na kumpelekea kuweza kuwa mshindi namba 3 katika shindano hilo, pia ametoa wito kwa wazanzibari kuweza kushiriki shindano hilo kwa wakati ujao kwani shindano ni zuri na linachangamoto kubwa kwa watu wenye umri kama wake.
Thursday, August 30, 2012
WAMACHINGA WANASAIDIA....
Wamachinga wakiwa wamepanga biashara zao pembezone mwa barabara kubwa ya magari maeneo ya kituo bangi (Tanga)
Wamachinga wakiendelea kufanyabiashara zao katika kituo cha daladala Darajani Zanzibar
Mara nyingi serikali imekuwa ikipiga kelele juu ya wafanyabiashara hao kuwa wawe na sehemu maalum ya kufanyia biashara hizo na kuwatengea maeneo yanayostahili kuwapo. Lakini mbali na kutengewa maeneo wafanyabiashara hao hawapo tayari kuyatumia maeneo hayo wakihofia hawawezi kuwapata wateja wanaowategemea katika biashara zao.
Ni kweli wamachinga ni msaada kwa watu kwa maeneo wanayoyatumia ikiwa ni Stendi za mabasi , vituo vya daladala na pembezoni mwa barabara kwani wanawarahisishia wasafiri kupata mahitaji kwa ukaribu zaidi.
Tatizo kubwa linalopelekea kuwa ni kero kwa watu ni ile hali ya wafanyabishara hao kutumia maeneo ya watembea kwa miguu barabarani kuweka biashara zao hali inayohatarisha maisha ya watembea kwa miguu kwa kukosa sehemu ya kupita na kusababisha wapite barabara kubwa yanapopita magari. Kwa upande wa vituoni wanapelekea msongamano usio kuwa wa lazima na kusababisha hali ya wizi kuongezeka.
Baada ya kuonekana hayo kuna haja ya serikali kuangalia namna nyingine ya kuweza kuwasaidia wafanyabiashara wa namna hii ambao wapo karibia Tanzania nzima.
Tuesday, August 28, 2012
ALI NAHODA MTANGAZAJI WA KIPINDI CHA "RAHA UTAMU" COCONUT FM
Mtangazaji wa kipindi cha Raha Utamu Ali Nahoda
Kama unasikiliza Coconut Fm 88.2 hapo ulipo utakua unapata burudani ya nyimbo za Taarab za taratibu kidogo kupitia kipindi cha Raha Utamu ambacho ndio kipo hewani mda huu.
Ali Nahoda ndio anatoa vitu vitamu kwelikweli kupitia mawimbi ya Mambo ya Zenji kila siku ya jumatatu hadi ijumaa.
A DAY IS NICE
Show 5 akiwa na Diva Rayshizzle katika Run the Beat
Show 5 Yoram akiwa ametupia ile mbovu
Rayshizzle na Hamida Maalim
Dj dr B na mwanadada Rayshizzle
Hamida Maalim na Dj Dr B
Diva wa Fleva 145 Rayshizzle (Queen of afternoon showz)
Sunday, August 26, 2012
DJ DR B NIMEAMUA KUACHA KAZI COCONUT FM
Dj dr B
Maisha ni safari ndefu sana ambayo mwisho wake ni mwisho wa uhai wako, Pamoja na kuwa maisha ni safari ndefu, hakuna safari inayokosa kituo ni sawa na kwa upande wangu tarehe 30/08/2012 safari yangu ya maisha ya Coconut yanafikia kituo. Nimeamua kuacha kazi kwa sababu zangu binafsi na kupumzika kwa muda nikiwa najipanga kwa mambo yangu mengine..
Najua wengi watatamani kujua sababu nimeamua kufanya hivyo kwaswababu zangu binafsi sina tatizo lolote na ofisi yangu na ninaipenda sana.
Vikwazo na misukosuko ni moja ya njia ya maisha ya mwanadamu tusameheane kwa pale tulipokwenda tofauti na kuangalia maisha mtazamo wa kimaendeleo. Nahitaji ushirikiano wako uendelee kuwapo kama kawaida kwa lolote na popote tuwe pamoja.
Najua wengi watatamani kujua sababu nimeamua kufanya hivyo kwaswababu zangu binafsi sina tatizo lolote na ofisi yangu na ninaipenda sana.
Vikwazo na misukosuko ni moja ya njia ya maisha ya mwanadamu tusameheane kwa pale tulipokwenda tofauti na kuangalia maisha mtazamo wa kimaendeleo. Nahitaji ushirikiano wako uendelee kuwapo kama kawaida kwa lolote na popote tuwe pamoja.
COCONUT FM,
ZANZIBAR,
C.E.O
PRIME TIME PROMOTION
S.L.P
DAR -ES- SALAAM
K.K
MENEJA,
COCONUT FM,
ZANZIBAR.
YAH: TAARIFA YA KUSITISHA MKATABA
Tafadhali husika na mada ya hapo juu.
Dhumuni la barua hii ni kuiarifu Kampuni kuwa kutokana na sababu binafsi nimeamua kusitisha mkataba wangu wa kazi kuanzia Agasti 30.2012.
Baada ya kuitumikia Primetime Promotion Ltd kupitia kituo chake cha redio Coconut Fm kwa takribani miaka mitatu na nusu, kwa matakwa yangu binafsi pasipo kushawishiwa na mtu yeyote nimeamua kuacha kazi.
Nashukuru kwa ushirikiano ambao nimepata kutoka kwa uongozi wa Coconut Fm pamoja na Primr time Promotion ,wafanyakazi wenzangu wa Coconut Fm, Prime time Promotion na baadhi ya wafanyakazi wa Clouds Media group kwa kipindi chote ambacho tumekuwa pamoja, nashukuru nimeamua kuondoka kwa amani na ninaamini Kampuni haitosita kunipokea endapo nitahitaji kurudi kufanya kazi na Prime Time Promotion.
Mwisho nawatakia kila la kheri katika harakati za kusukuma mbele gurudumu la maendeleo la Coconut Fm na Prime time Promotions Ltd.
……………………..
Mbaraka Saidi Boha
Saturday, August 25, 2012
"HAIKUWA RAHISI" - SOLID BLACK & MUT LOW
Ramyson Madoro akiwa katika kipindi cha Shusha Fleva
Ramyson Madoro katika Shusha Fleva akizungumza na Solid Black pamija na Mut Low washkaji walioamua kuacha uteja na kuingia kwenye sanaa ya muziki kuielimisha jamii
Solid Black
Mut Low
Kutoka kulia ni Ramyson Madoro,Mut Lowa na Solid Black wakishow love baada ya kumaliza mahojiano kwenye Shusha Fleva.
Haikuwa Rahisi kama ngoma yao inavyoitwa kwa hawa jamaa Solid Black na Mut Lowa kuweza kuachana na hali ya utumiaji wa madawa ya kulevya kwa kipindi cha miaka 7 hali iliyopelekea kupoteza muelekeo wa maisha yao kwa kipindi chote walichokuwa wakitumia madawa ya kulevya.
Black na Mut baada ya kushauriwa kuacha kutumia madawa ya kulevya waliishi Souba house kwa muda wa mwaka mmoja wakiwa na wenzao waliokuwa tayari kuacha kutumia madawa kulevya.
Wameamua kuingia kwenye sanaa ya muziki wa bongo fleva kwa lengo la kuelimisha vijana wenzao kuachana na utumiaji wa mada ya kulevya.
Wimbo wao wa kwanza "Haikuwa Rahisi" walioufanyia studio za T-Top chini ya producer Chief Elia wamechanganya lugha mbili ikiwa ni kiswahili na kiingereza ili kwa yule ambae kiswahili kwake hakipandi ujumbe ataupata kwa lugha ya kiingereza, Solid Black amesimamia vema vesi yake kwa lugha ya kiswahili wakati Mut Low amechana kwa lugha ya kiingereza.
Skiliza ngoma hiyo uone ujasiri wa washkaji kutoka kwenye uteja hadi usanii.....
Solid Black & Mut Low - Haikuwa Rahisi
Friday, August 24, 2012
TEN YEARS LATER (Letter to Dandu)
Mambo vp! Jumatatu ya tarehe 27, August, 2012 ni miaka kumi tangu kifo cha marehemu James Maligisa Dandu aka "Mtoto wa Dandu" ama CJ Massive, aliyefariki kwa ajali ya gari jijini Dar es Salaam, August 27, 2002. J apo ni kama vile watu wameanza kumsahau lakini mimi sitoweza kumsahau kamwe. Aliniinspire sana kufanya muziki. So wiki hii mpaka ijumaa nimeamua niitumie kutafakari mazuri aliyoyafanya kwenye muziki wa Tanzania na nimemwandikia barua hii ambayo pia ina wimbo wake hapo kwenye attachment.
This time nipo Dar city, the Hustles city
August 27, 2002 with a fatal accident, shujaa ukawa umeaga
Ten years later the game is still strong
New Artists, new flows new production
Rap bado ipo ila kiduku ndio fashion
Wanauita muziki wa hela hawaaimbi kwa passion
Muziki yes unalipa vijana wanadrive tu
Gari za maana wachache wamestay true
Show za laki laki humpati huyo Diamond
Humpati AY humpati hata Saigon
Clouds bado wapo watemi kama kawa
Wanapiga tu mahela Fiesta kama dawa
Bongo Records bado ipo ila P-Funk simwelewi
Majani sio Majani, sio Kinywele kimoja tena
Ameshalose focus MJ ye anapeta
Piga sana mkwanja commercial mpaka noma
BSS, matangazo Airtel mpaka Voda
Mchizi yuko safi dread zake safi
Vp maisha ya heaven? Hope it’s all good
Dunia bado mbovu no money no food
Somalia, Eritrea DR Congo
Hakuna maisha bora shida tu hata Bongo
CCM sio shwari this time wanaenda down
CHADEMA wako hot wanaweza chukua hiyo crown
Ufisadi bado upo wa Radar mpaka Dowans
Story zile zile nightmare za Darwin
Siasa na vijana inashika kwa kasi
Sugu ndani ya mjengo alipata nafasi
Zitto, January yule mtoto wa Makamba
Mnyika, Tundu Lissu hawa jamaa wanatamba
Kifupi Tanzania imeshachange sana man
Thanks to the lord bado tunayo amani
Ujinga na maradhi bado tatizo bado lipo
Tumuombe Mungu tuje tuonane tena my brother
Niaje Dandu, Sky hapa tena, nataka kuholla tena
Last time nilikuwa Rock City, your home CityThis time nipo Dar city, the Hustles city
August 27, 2002 with a fatal accident, shujaa ukawa umeaga
Ten years later the game is still strong
New Artists, new flows new production
Rap bado ipo ila kiduku ndio fashion
Wanauita muziki wa hela hawaaimbi kwa passion
Muziki yes unalipa vijana wanadrive tu
Gari za maana wachache wamestay true
Show za laki laki humpati huyo Diamond
Humpati AY humpati hata Saigon
Clouds bado wapo watemi kama kawa
Wanapiga tu mahela Fiesta kama dawa
Bongo Records bado ipo ila P-Funk simwelewi
Majani sio Majani, sio Kinywele kimoja tena
Ameshalose focus MJ ye anapeta
Piga sana mkwanja commercial mpaka noma
BSS, matangazo Airtel mpaka Voda
Mchizi yuko safi dread zake safi
Vp maisha ya heaven? Hope it’s all good
Dunia bado mbovu no money no food
Somalia, Eritrea DR Congo
Hakuna maisha bora shida tu hata Bongo
CCM sio shwari this time wanaenda down
CHADEMA wako hot wanaweza chukua hiyo crown
Ufisadi bado upo wa Radar mpaka Dowans
Story zile zile nightmare za Darwin
Siasa na vijana inashika kwa kasi
Sugu ndani ya mjengo alipata nafasi
Zitto, January yule mtoto wa Makamba
Mnyika, Tundu Lissu hawa jamaa wanatamba
Kifupi Tanzania imeshachange sana man
Thanks to the lord bado tunayo amani
Ujinga na maradhi bado tatizo bado lipo
Tumuombe Mungu tuje tuonane tena my brother
Thursday, August 23, 2012
Wednesday, August 22, 2012
DJ DR B AM BACK IN UNGUJA
Nimerejea Unguja leo asubuhi na boat ya Kilimanjaro III baada ya kumaliza mapumziko yangu ya mwezi mtukufu wa ramadhani ambayo nimeyamalizia nyumbani kwetu Tanga kunani. I thanks Gog nimefika salama
NILITEMBELEA SHAMBA LETU LILILOPO MICHUNGWANI TANGA
Nikiwa pembeni kidogo ya shamba nikiwaonyesha vibarua mpaka wa kuishia wakati wakilima
Kwa bahati nzuri nilipokuwa nipo nyumbani kwetu Tanga wiki moja baadae baada ya kuwa tayari nimepata nafasi ya kutembelea ndugu na jamaa nilipanga safari ya kwenda kutembelea shamba letu lililopo Michungwani. Furaha kubwa nilikuwa nayo baada ya kufika shambani hapo kwani ni miaka mingi sikuwahi kwenda na mambo mengi nilikuwa nayapata ambayo yalikuwa yakinisikitisha sana, kwa shamba ni hali ya kawaida kusikia mtu analima shamba la mwenzie bila ruhusa na hilo ndilo lilikuwa likilikabili shamba letu.
Nashukuru kwa sasa shamba liko salama na maandalizi ya kilimo cha mwaka huu yameanza kama unavyoona.
Kwa bahati nzuri nilipokuwa nipo nyumbani kwetu Tanga wiki moja baadae baada ya kuwa tayari nimepata nafasi ya kutembelea ndugu na jamaa nilipanga safari ya kwenda kutembelea shamba letu lililopo Michungwani. Furaha kubwa nilikuwa nayo baada ya kufika shambani hapo kwani ni miaka mingi sikuwahi kwenda na mambo mengi nilikuwa nayapata ambayo yalikuwa yakinisikitisha sana, kwa shamba ni hali ya kawaida kusikia mtu analima shamba la mwenzie bila ruhusa na hilo ndilo lilikuwa likilikabili shamba letu.
Nashukuru kwa sasa shamba liko salama na maandalizi ya kilimo cha mwaka huu yameanza kama unavyoona.
Saturday, August 4, 2012
BONYFACE aka HANDSOME BOY AACHIA NGOMA MPYA TOKA “MENSEN SELECTA”
Bonyface a.k.a Handsome Boy
Msanii huo ambae yupo katika Lebo ya Mensen Selecta Deffetarty Music kwa sasa yupo chimbo pamoja na producer wake kupakua mawe mengine ambayo yataachiwa hivi karibuni.
Bonyface a.k.a Kidume ameweka wazi njia za mawasiliano yake ili yeyote mwenye ushauri na maoni kwake aweze kufunguka kupita nambari yake ya simu facebook au email yake kwa lengo la kukuza muziki wa bongo:
Simu : 0715 600750
Email:- bonyface.mateza@yahoo.com
Facebook:- bonyface.mateza@yahoo.com
Subscribe to:
Posts (Atom)