Thursday, January 31, 2013

"ROHO MBAYA" TOKA KWA SAJNA YATIKISA KITAANI

"Ni kitambo kirefu sana nimekuwa kimya kutokana na maswala ya shule ila sasa kidogo nimetulia. Nimeamua kuuachia wimbo huu unaitwa ROHO MBAYA ambao nimewashirikisha BELLE 9 na PIPI kama zawadi yangu kwa fans wangu, lakini official single ya mwaka huu inafuata siku si nyingi. 

Wimbo huu beat ilifanywa na Duke wa M-Lab na vocals zilifanywa na Tetemesha Records mwaka juzi".

"Tegemeeni mengi mazuri kutoka kwangu kwa mwaka huu".
Hayo ni maneno yake Sajna aliyoyazungumza siku chache baada ya kusambaza ngoma yake mpya kupitia zeetown email. 
Wengi mnamfahamu Sajna kwa ngoma zake kali zinazopendwa kila kona kama vile Mganga na nizingine mpango wake sasa umekaa fresh baada ya kubwanwa kwa muda na kitabu kama alivyozungumza. Tetemesha Rc ni studio pekee iliyoweza kumtambulisha vizuri sana Sajna katika game la muziki wa kizazi kipya Producer Kid Bway akiwa ndio msababishaji.

CRISS ^ PADDY MAUZO CLASSIC

My hope you are well as you are reading this mail now. I have attached a New Song from upcoming Bongo flava Artist from Tanga who are very talented and trying hard to make their way to the top. Together me and you we can make it possible for them simply by giving our sincere support.

I present to you Criss ft Paddy with their new Song "Niambie". Below are the song details

Song Details
Artist         :  Criss ft Paddy
Song         :  Niambie
Studio       :  International Quality
Producer   :  JB

Huu ndio ujumbe alionitumia msela nami naufikisha kwako kama ulivyo ili uweze kutoa sapoti ya ukweli kwa mchizi

MAN TO MAN CONNECTION WAACHIA NGOMA MPYA YA SHEBBY LOVE

MAN TO MAN CONNECTION  WAACHIA NGOMA MPYA YA SHEBBY LOVE
Toka pande za tandale namtambulisha msanii mpya  ambaye jina lake lipo midomoni mwa  wapenzi wa muziki wa kizazi kipya kwasasa. Baada ya Man to Man Connection kuanza kuachia nyimbo zake…….Shebby love  a.k a. “handsome boy”  ni msanii mwenye mafanikio lukuki tangu awe anafanya kazi pamoja na  Ney wa mitego, ingawa sasa hivi Shebby  love amesimama peke yake kama Shebbyl ove chini ya  meneja wake Man to Man Connection. Wimbo  mpya wa Shebby love unaitwa “KIPATO BADO” kazi mzima ikiwa imefanywa na studio ya Pure Record ya mjini morogoro  chini ya usimamizi wa watu wawili makini “Dizzy mchizi” pamoja na “hits beats” kazi ni ya uhakika ile mbaya wimbo ukiwa kwenye mandhari ya “mnanda”. Video ya wimbo huu tayari  inafanya vizuri kwenye vituo mbalimbali vya runinga hapa Tanzania , kazi kwako wewe shabiki wa muziki wa kizazi kipya……..ebu sikiliza track hii kisha utaamini kuwa kazi imefanyika katika kuandaa voko pamoja na mpangilio mzima wa beat.

Msanii                    :         shebby love
Wimbo                   :         kipato bado
Studio                   :         Pure Record Morogoro
Producer                :         Dizzy Mchizi & Hits beats
Namba ya simu       :         0719 121415
Facebook               :         shebby love

BIBO ACHOMOKA KIMPANGO WAKE

Mambo vipi Wadau?
Huyu Hapa Climax Bibo Kutoka kwenye Kundi la Mexicana Lacavela ambaye sasa ameamua kufanya kazi zake Nje ya Kundi hilo linalosemekana limevunjika (habari zisizo rasmi) hapa Climax yupo chini ya Music Label Mpya ya Benjamin Wa Mambo Jambo BML Productions, ikiwa ni mkono wa benjamin busungu, support Muziki wetu share this to People jina la Wimbo Geto Boy, Studio BML Productions, Producer Benjamin Busungu..
Pamojah,
Benjamin
kutoka zeetownblog

Wednesday, January 30, 2013

BRAND NEW JIWE TOKA KWA LINEX

Ukizungumzia  mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya mwenye sauti ya pekee  (Personal Identity) mwenye mashairi yaliokwenda shule na yanayogusa hisia  na maisha ya kawaida ya kila siku hasa kwenye maswala ya mapenzi …. Na inasemekana ni msanii anayeongoza kwa kupendwa na wanandoa wengi hapa bongo kutokana na jinsi mashairi yake yanavyowagusa hasa wanandoa ndani ya nyumba…..ni msanii pekee wa bongo fleva ambaye anawagusa sana watu wazima kuliko msanii mwingine yeyote wa bongo fleva………. na  si mwingine ni Linex ..!..... hivi punde tu ametoka kuachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la MAHAKAMA YA MAPENZI……….. wimbo umetengenezwa Sweden kwa Fundi samweli sauti imerekodiwa na tuddy Thomas, kwahiyo uandaaji mzima wa wimbo umefanywa na producer  Fundi  samweli (mzungu)  ebu sikiliza  wimbo huu jinsi fundi alivyopangilia muziki huo kwa ustadi wa hali ya juu.
MSANII                         :      LINEX
WIMBO                         :      MAHAKAMA YA MAPENZI
MTAYARISHAJI               :      FUNDI  SAMWELI (FROM SWEDEN)
MTAYARISHAJI WA SAUTI :      TUDDY THOMAS

NEW SINGLE THE MASSAGE

Track mpya ya bac-t pamoja na Mani martin inaitwa The Massage,  ni track inayo zungumzia story ya kaka na mdogo wake, Mdogo anampenda Demu kaka ana mkataza akidai kuwa demu ana tabia mbaya, ila mdogo hataki kuskia amezama ki mapenzi.
Imetengenezwa na Producer DJB, ndani ya  studio za BigTown Records nchini Rwanda- Kigali.