Sunday, February 17, 2013

NEW AUDIO: LADY ZHENA - MWANAUME

Lady Zhena
Lady Zhena ni Mwanadada ambaye alitambulika katika game takriban miezi miwili iliyopita...mara baada ya kutoka na ngoma inayokwenda kwa jina la "Nieleze" akimshilikisha B. Barozi katika studio ya Mazuu Rec. Lady Zhena sasa amekuja kivingine katika mahadhi ya kwaito katika ngoma inayokwenda kwajina la "MWANAUME" ikifanyika katika studio za Mazuu Rec. Kwa ufupi ni mwanadada ambaye amedhamiria kutamba katika ngoma tofauti tofauti, huku akibainisha yeye kama binti amejipanga kuwa level ya juu.

Lady Zhena anatabaisha kuwa kimsingi bado hajaona kazi za artist wa kike zikifanya vizuri, ukimuweka pembeni mwanadada Lady Jay dee ambaye ndiye kivutio chake na mwenye mafanikio.

Anasema yeye atahakikisha muziki wa kizazi kipya kwa akina dada unapaa juu, huku akitaadhalisha vijana wa kiume wajipange kushushwa.

Lady Zhena hivi sasa yuko kwenye maandalizi ya kutoa video ya wimbo wake mpya MWANAUME, video ambayo amenadi kuwa ya kiwango cha hali ya juu, kuanzia kwenye production, location, dressing na muonekano mzima wa video hiyo utakuwa wa tofauti.

Maudhui ya wimbo MWANAUME ni kwamba Mume amemtelekeza Mwanamke na watoto, bila ya mahitaji ya nyumbani, Mwanaume kaondoka hajulikani alipo, nyumbani shida tupu.

AKUDO IMPACT - WAZEE WA MASAUTI KUTUMBUIZA SHINDANO LA TAIFA MISS UTALII TANZANIA 2012/13 – VIPAJI


Taarifa kwa Vyombo vya Habari – 12-2-2013
AKUDO IMPACT - WAZEE WA MASAUTI KUTUMBUIZA SHINDANO LA TAIFA
MISS UTALII TANZANIA 2012/13 – VIPAJI
Bendi ya Akudo Impact wazee wa masauti ,siku ya Jumapili tarehe 17, Februari 2013, itatoa burudani katika shindano la Taifa la kumsaka Mrembo wa Utalii mwenye kipaji kati ya warembo 40 waliopo kambini Ikondelelo Lodge wakijiandaa kushiriki Fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania 2012/13 zitakazo fanyika mwisho wa mwezi huu katika Ukumbi wa Dar Live jijini Dar es Salaam.

Katika shindano hilo la Vipaji , ambalo litafanyika katika Ukimbi wa Jeshi wa Msasani Beach Club Jumapili kuanzia saa nane mchana ,pamoja na Bendi hiyo ya Akudo Impact , wasanii wengine watakao tumbuiza ni pamoja na mwanamuziki wa kimataifa Che Mundugwao, Msanii mdogo chipukizi wa muziki wa kizazi kipya Geneous na burudani za ngoma za asili kutoka katika kundi kongwe la Kaole  Sanaa Group wakiomgozwa na mwana dada mahili katika uchezaji wa ngoma za asili Mariam Kweji aka kalunde wa Bongo Movie.Shindano hilo la Vipaji ni moja ya mashindano ya awali ya kuwania tuzo mbalimbali kabla ya Fainali kuu,ambapo washiriki wote watashindana kuimba na kucheza nyimbo na ngoma za makabila mbalimbali ya mikoa wanayo iwakilisha. Mikoa hiyo na majina ya washiriki katika mabano ni  Arusha (Rose Godwin), Dar es Salaam 1 (Sophia Yusuph),Dar es Salaam 2(Ivon Stephen),Dar es Salaam 3 (Irine Thomas),Dodoma (Erica Ekibariki), Geita (Hamisa Jabiri), Iringa (Debora Jacob), Kagera 1(Elline Bwire),  Kagera2 (Jania Abdul), Kagera 3(Mulky Uda),  Kilimanjaro (Anna Pogaly), Lindi (Joan John), Mtwara (Halima Hamis),Mara (Dorine Bukoni), Manyara (Mary C. Lita), Mbeya (Diana Joachim), Mwanza (Jesca Peter), Morogoro (Hadija Said),Tanga (Sarafina Jackson), Ruvuma 2 (Leah Makange), Tabora (Magreth Malalle), Njombe (Pauline Mgeni), Rukwa (Anganile Rogers), Katavi (Asha Ramadhani ), Simiyu (Flora Msangi), Shinyanga (Lightness Kituwa), Ruvuma (Furaha Kinyunyu), Kigoma 1(Zena Ally), Kigoma 2(Rosemary Emmanuel), Pwani (Beatrice Iddy), Singida (Neema Julius), Singida (Christina Daud),Vyuo Vikuu (Irine Richard), Vyuo Vikuu (Hawa Nyange)

Wakizungumzia kwa nyakati tofauti shindano hilo la Vipaji,Rais wa Miss Tourism Tanzania International Organisation ,wenye dhima ya kikomo ya kuandaa na kuendesha mashindano hayo , alisema kuwa mandalizi karibu yote yamekamilika kuanzia ngazi za warembo hadi burudani za bendi, ngoma za asili na muziki wa kizazi kipya. Hili litakuwa ni tukio kubwa na la kihistoria kuwahi kufanyika Tanzania ambapo Utalii, Urembo na Utamaduni wa ngoma za asili vitaonyeshwa kwa pamoja jukwaani, lakini kivutio cha pekee ni jinsi mabinti wa kizazi kipya tena warembo kutoka mikoa yote ya Tanzania na vyuo Vikuu watakavyo onyesha maajabu ya kusakata ngoma za asili kwa umahili mkubwa na wa pekee.Shindano la Miss Utalii Tanzania mwaka huu limedhaminiwa na wadhamini mbalimbali wakiwemo Coca Cola Kwanza Limited, Daja Salon, Mtwana Catering Services Enterprises, Zizzu Fashion, Global Publishers, Ikondelelo Lodge, Clouds Media Group, Tone Multimedia Group, Oriental Bereau Dechange Valley Spring na www.misstourismorganisation.blogspot.com

Katika Shindano hili viingilio vitakuwa ni kama ifuatavyo 5,000 kwa viti vya kawaida, 10,000 kwa V.I.P 2, na 30,000 kwa V.I.P 1 pamoja na Chakula.
MAELEZO YA PICHA: PICHA 1,2 WASHIRIKI WA MISS UTALII TANZANIA 2012/13 WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA
Asante,

Erasto G. Chipungahelo
Rais

Msanii chipukizi Ramadhan Jumanne

Msanii chipukizi katika medani ya BongoFleva Ramadhan Jumanne aka 4R toka pande za singida aja na nyimbo yake ya kwanza kabisa aloipa jina "Kutonipenda" ikiwa ni Zouk-rnb alorecodi studio za noizmekah Arusha. anataraji kufanya ngoma nyingine inayokwenda kwa jina "Si ungeniambia" hapo badae lakini kwanza support "Kutonipenda" kwa kubofya HAPA .kwa mawasiliano ya mahojiano, matamasha na mengineyo wasiliana na 4R kwa simu +255 766 141 566

NEW MZUKA MAGAZINE COVER

Hili ni cover la jarida jipya la Mzuka.

Friday, February 8, 2013

Jambo Squad na Almando Lady Fire na Tendo

Maalmando wa JamboSquad wafungua mwaka kwa "TENDO",pini la Amando Lady Fire alodundia pande za noizmekah.com huku verse ya pili na ya tatu zikishikiliwa na Ordinally pamoja na NiggaC, Download HAPA na endeleza support kwa muziki wa Tanzania. kwa mawasiliano zaidi/Bookings na interview bonga na LadyFire kupitia +255 758 395 797

Baada ya kuenjoy Video Release sasa pata official Audio Release ya wimbo wa msanii BeeMan toka Love Child Records Nairobi,Embe Dodo

 
Baada ya kuenjoy Video Release sasa official Audio ya wimbo wa msanii BeeMan toka Love Child Records Nairobi,Embe Dodo nao umedondoshwa rasmi katika vituo mbalimbali vya Redio Afrika Mashariki.



the outburst

Msanii Kinda toka Outburst Gangstaz ya A-City, Wise D "BOSCO", Aja na track mpya BETTER DAY.
Producer: Grandmaster Records
DOWNLOAD LINK HULKSHARE: http://hu.lk/wees5fb9jls0

Benjamin Wa Mambo Jambo's New Song

Hi Every One,
This is My new Release, it has been long time now, and i am sure my Fans miss to hear something from me, here i come again and i know how important you guys are to me, i please you to share and promote my song to your Blogs,Websites,News papers ,Radios, Clubs,Bar,restaurants,Hotels and everywhere you know or think is possible,this song composed,produced,editedet and mixed by Benjamin Busungu myself for Bml Productions(my new Studios & Music Label) and the Video coming out soon, i promise to breaf when comes out, i re-pleased you to share it feel free to ask if needed,
thanx a lot,
Benjamin wa Mambo jambo,
CEO BML Productions
2013

Name of The Song - Skendo(Scandal)
Artist - Benjamin Wa Mambo Jambo
Studio - BML Productions
Producer - Benjamin Busungu
Genre - Afro Ragga
Lengh - 4:13
Bpm - 100

ManBatoo na "She nah leave"

Pata riddim track toka kwa ManBatoo aka Rudbwai from Arachuga Kijenge juu,Reggae joint inakwenda kwa jina "She nah leave" ikiwa ni new years release juu ya "heart & soul riddim" na mixing pande za www.noizmekah.com. Bofya HAPA and Enjoy

Tuesday, February 5, 2013

Lady Yoo toka Sanawari Arusha

Binti mwenye umri mdogo ulioambatana na kipaji kikubwa katika kughani anayekwenda kwa jina Lady Yoo, anadrop brand new single "lady yoo" ilosukwa pande za noizmekah.com ikiwa ni hardcore hiphop track inayomtambulisha mwanadada rappa katika game.sikiliza na kudownload HAPA na kwa mawasiliano zaidi kuhusu mahojiano na Bookings na Lady Yoo check +255 758 394 470

WANA SKYLIGHT BAND

Hey...
Nadhani kuna kila sababu ya kutoa ushirikiano kwenye muziki wa dansi ambao inaaminika umedrop sana.
Skylight band ni moja wapo baina ya Band mpya ambazo muelekeo wake umekuwa ni mzuri sana kiasi
kufikia hatua ya kujikusanyia idadi kubwa ya mashabiki hasa wale wapenzi na mashabiki wa muziki wa dansi nchini
So kama mtanzania unapaswa kutoa ushirikiano wa hali na mali katika kuunyanyua muziki wa dansi ukiwa na sura mpya.
Hawa ndio wana Skylight ambao sasa wanatamba na songi la Carolina,

BRAND NEW: C-SIR MADINI - NDAGU (2013)

Kazi mpya ya mwaka huu ya msanii C-SIR MADINI inayoitwa NDAGU akiwa amemshirikisha JOSEFLY sasa imedondoka kitaani.

Wengi mtakuwa mnajiuliza why mchizi ameuita wimbo huo 'NDAGU' kwa upande wa wasukuma naamini sio neno geni kwao ila ipo sababu ya kushangaa pia kwakuwa inaeleweka maana ya neno hilo kwa upande wao, Mchizi kafunguka maana ya hilo neno na alivyomaanisha katika stori ya wimbo alioupa jina la ndagu akiwa yeye mwenyewe ndio song writter.

'NDAGU' ni neno la kisukuma linalomaanisha Kafara, hivyo story ya wimbo huu inazungumzia watoto wa familia moja walioamua kuukataa utajiri wa familia yao, baada ya kugundua utajiri huo umetokana na baba yao kumtoa kafara mdogo wao mmoja.

Offcoz Ni wimbo wenye ujumbe unaogusa maisha ya watu wengi kutokana na hali halisi ya uwepo wa mambo hayo katika baadhi ya familia.

Bico ft DX katika Mo dan Faya

Click link kupata wimbo mpya wa RaggaDancehall artist BICO toka arachuga katika pini la Mo dan Faya alomshirikisha producer DX katika chorus, download HAPA na kwa mawasiliano na mzee mzima Bico kwa mahojiano na Bookings check nae kupitia digits +255 766 430 285