Saturday, July 20, 2013

Miili ya Askari Saba waliofariki huko Darfur yawasili nchini leo

Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi
wa Tanzania (JWTZ) wakipakia moja ya
masanduku saba yenye miili ya askari
wa jeshi hilo waliofariki dunia huko
Darfur nchini Sudan wakati wakilinda
amani, baada ya kuwasili kwenye
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam leo
alasiri.
Miili ya Askari saba wa Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania
(JWTZ) waliofariki Dunia wakati wakiwa
katika kazi ya kulinda amani kwenye Mji
wa Darfur nchini Sudan,imewasili nchini
leo majira ya alasili kwa kutumia ndege
maalumu ya Umoja wa Mataifa.
Askari hao waliuwawa kwa shambulio
la kushtukiza na kundi la waasi wakati
wakiwa kwenye kazi yao ya kulinda
amani nchini Sudan.
Jeshi la JWTZ lilitoa taarifa likisema
kuwa tukio hilo ni pigo kubwa kwa nchi
ya Tanzania ikiwa ni la kwanza kutokea
tangu Tanzania ilipoanza kuchangia
walinzi wa amani chini ya Umoja wa
Mataifa mwaka 2007.

Published with Blogger-droid v2.0.10

No comments:

Post a Comment