Saturday, July 28, 2012

SHOPING YANGU NCHINI UGANDA

Nikiwa shoping nilipokwenda kutembea nchini Uganda
Moja picha ya kihistoria iliyowekwa kama kumbukumbu nchini Uganda nilibahatika kupiga nayo picha

Friday, July 27, 2012

SUMA LEE ACHOMOKA NA "APATE RAHA"

Alianzia na Chungwa zikaja nyingine kadhaa kama Rafiki balaa likaja kwenye Hakunaga ikafuata Utanikumbuka na sasa SUMA Lee ametoka na SINGO yake mpya Inayokwenda kwa jina la APATE RAHA Mkono wa Maneke ndani ya AM Record kama kawa sikiliza balaa hilo hapa

MANDOJO NA DOMOKAYA WAVUNJA UKIMWA WACHOMOKA NA BRAND NEW TRACK "NILIMUONA"

Wengi mnaposikia Mandojo na Domokaya mnakumbuka enzi za Niaje, hawa jamaa waliweka historia kubwa katika game la muziki wa bongo fleva kwa ngoma zao kali zilizotamba kila kona.

Ukibahatika kuwaona kitaani mara nyingi utawaona wamebeba magita yao mabegani. Hii ni kuonyesha kwamba muziki kwao ni popote na tungo zao hawatungi bora kutunga wala sio wanachokiona tu bali ni hadithi za kweli za maisha yao wenyewe kitu ambacho ni vigumu kuwatenganisha utapomouna Dojo pembeni Domo kaya.


Baada ya kimya cha muda mrefu wakali hawa kutoka kundi la Wamandavaku kutoka mkoa wa Arusha wameamua kuvunja ukimya kwa kuchomoka na singo yao mpya inayoitwa Nilimuona.
Kazi imefanywa na na Prducer Tuddy Thomas. isikilize hapo chini kweli jamaa wamejipanga
Mandojo - Domo Kaya - Nilimuona

DIAMOND APAGAWISHWA NA VIDEO YA LINEX - AIFOLA

Diamond
Diamond afungua hisia zake kwa video ya Linex - Aifola kuwa hii ni moja kati ya nyimbo anazozipenda sana toka nchini kwake Tanzania, "Kuanzia Tittle ya Ngoma Mellody, Sauti Hadi maneno yaliyoandikwa humo pia navutiwa sana na ubunifu mzuri wa lugha ya KIHA aliyoichanganya Linex kwa ufundi mkubwa ndani ya nyimbo hii"
Hayo alifunguka Diamond baada ya uzalendo kumshinda katika kuzuia hisia zake alichokifanya kupitia mtandao wake This is Diamond ametupia video hiyo na kueleza kile kile ambacho kimemvutia katika wimbo huo.
Mbali na hayo Pletnum aliongeza kusema kuwa "Yote tisa na kumi ni BEAT kali yenye Hisia nyingi sana iliyotengenezwa na FUNDI SAMWELI producer toka Sweeden.. na kwataarifa yako Linex amentumia beat ya nyimbo hii na Nimeiandika nyimbo moja kali saaanaaa........SOON UTAISIKIA" huo mpango unaoendelea kwa Diamond.

Thursday, July 26, 2012

MV KALAMA, MV SEPIDEH NA MV SEAGUL ZAFUTIWA HATI YA KUFANYA KAZI ZANZIBAR


Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar Abdullah Husein Kombo

Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar imezifutia rasmi hati ya kufanya kazi Meli ya Mv.Kalama, Mv.Seagul na Mv.Sepideh kutokana na meli hizo kutokukidhi hali ya usalama wa abiria katika meli hizo.

Aidha meli hizo zimepewa muda wa mwezi mmoja kuanzia leo kuhakikisha zimeondoka katika maeneo ya Zanzibar kabla ya hatua zaidi kuchukuliwa dhidi ya wamiliki wa Meli hizo.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar Abdullah Husein Kombo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Afisini kwake kuhusu hali ya usafiri wa baharini na usalama Zanzibar.

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR NA VIKOSI VYA ULINZI WAPONGEZWA.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Mkuu wa Mabalozi wa Nchi za Nje waliopo Tanzania Bwana Juma Alfan Mipango hapo Ofisini kwake Baraza la wawakilishi Mbweni.
Pembani yao ni Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu { UAE } Bw.Mallallah  Mubarak Alameri.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  akizungumza na Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pencheni wa PPF Bibi Lulu Mengele aliyefika Zanzibar kutoa mkono wa pole kwa niaba ya Uongozi wa Mfuko huo kufuatia ajali ya meli ya hivi karibuni karibu na Kisiwa cha chumbe Zanzibar.

Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pencheni { PPF } Bibi Lulu Mengele akiwasilisha salamu za rambi rambi kwa Makamu wa PILI WA Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kufuatia ajali ya Meli ya M.V.Skagit iliyotokea wiki iliyopita.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akibadilishana mawazo na Bishop Michael wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Zanzibar mara baada ya kuwasilisha salamu zao za rambi rambi hapo ukumbi wa Baraza la wawakilishi Mbweni.
Pembeni ni Katibu Mkuu wa Dayosisi hiyo Bwana Nuhu Sallanya.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ushirikiano na Vikosi vya Ulinzi, pamoja na Taasisi za Kiraia imepongezwa kwa hatua  iliyochukuwa  katika kukabiliana na Maafa yaliyotokea ya kuzama kwa Meli ya M.V. Skagit wiki iliyopita.
Pongezi hizo zimetolewa na Uongozi wa Taasisi tofauti zinazoendelea kutoa mkono wa pole  hapa Zanzibar kufuatia vifo vya watu kadhaa waliokuwemo ndani ya Meli hiyo iliyopata ajali karibu na Kisiwa cha Chumbe.

NIAMINI NGOMA MPYA DOGO DITTO NI TUNU YA MAREHEMU MAMA YAKE MZAZI

Kwa mujibu ya maelezo ya Ditto,wimbo huu anautunuku kwa Marehemu Mama yake mzazi kwani Mama yake huyo aliupenda sana wimbo wa Niamini wa HBC.Na ndio sababu ya kupata wazo la kutunga wimbo huu, Mungu ailaze mahala pema peponi roho ya mama yake Ditto ameen. Usikileze wimbo huo hapa
                                           
                                         Lameck Ditto - Niamini 2012 Rnb version

 

Wednesday, July 25, 2012

CHAGUO NI LAKO


BI JAMILA ABDALAH AKIWA KATIKA FAZI LA KUJISTIRI

Bi Jamila Abdalah wengi wamezoe kumuita Baby J asema kuna baadhi ya waislamu ambao wanafikiri kufunga ni kutokula chakula tu kitu ambacho sio kweli na wanaofikiria hivyi basi hawahujui nini maana ya funga. Funga ni nguzo ya nne katika dini yetu hivyo lazima unapofunga utie nia na uwe na imani katika funga yako" alisema bi Jamila na kuwasisitiza wanawake wenzie kujistiri kama dini inavyotuambia na kufunya mema yanayompendeza M/Mungu.

SHABAN METAYA AKIPERUZI MAGAZETI

Kusoma magazeti kunasaidia kusogeza masaa mbele endapo swaumu imepanda, hapa bwana Metaya Shotgun kama anakazia ivi kwa kupitia habari mbalimbali kwenye gazeti.

Saturday, July 21, 2012

BODI YA MASHINDANO MISS UTALII YACHUKUA MAAMUZI MAZITO - YAFUTA SHINDANO

Washiriki Miss Utalii Kanda ya Ziwa .2012  
 
BODI ya Taifa ya Miss Tourism Tanzania Organization (MTTO), imelifuta
shindano la Miss Utalii Kanda ya Ziwa 2012, lililo fanyika New Mwanza
Hotel, juzi, huku taifa likiwa kwenye maombolezo ya siku tatu kutokana
na msiba mkubwa wa ajali ya meli ya Mv Skagit, mjini Zanzibar na
kupoteza uhai wa watu wengi.

Friday, July 20, 2012

DR SHEIN AWASISITIZA WAISLAM KUITUMIA MISKITI VIZURI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, amewasisitiza Waumini wa dini ya Kislamu kutoitumia misikiti kuwa vivutio vya kusababisha uhasama, malumbano au kuwafarakanisha waumini na watu wengine.
 
Alhaj Dk. Shein aliyasema hayo katika ufunguzi wa msikiti wa Rahmatullah uliopo Mwanyanya, Wilaya ya Magharibi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, ambapo viomngozi mbali mbali wa dini, vyama na serikali walihudhuria akiwemo Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Alhaj Ali Hassan Mwinyi.
 
Katika hotuba yake Dk. Shein alieleza kuwa  misikiti iwe kwa ajili ya ibada pamoja na kuendeleza elemu miongoni mwa waislamu.

KITAANI KIMENUKA

Askari akifyatua bomu la machozi kuwasambaratisha wanachi wanaofanya vurugu

COCONUT FM YAJIANDAA KWA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI

Meneja wa Coconut Fm ambae pia ni mtangazaji wa kipindi cha Nipe Nikupe akiwa katika pozi muda mfupi baada ya kuzungumza na watangazaji wake.

Wednesday, July 18, 2012

MY BLOG COMING SOON

MY FANS GET READY THIS IS THE BEST BLOG... B LIVE "B THE FIRST" COMING SOON