Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Mkuu wa Mabalozi wa Nchi za Nje
waliopo Tanzania Bwana Juma Alfan Mipango hapo Ofisini kwake Baraza la
wawakilishi Mbweni.
Pembani yao ni Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu {
UAE } Bw.Mallallah Mubarak Alameri.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
Ali Iddi akizungumza na Meneja Uhusiano
wa Mfuko wa Pencheni wa PPF Bibi Lulu Mengele aliyefika Zanzibar kutoa mkono wa
pole kwa niaba ya Uongozi wa Mfuko huo kufuatia ajali ya meli ya hivi karibuni
karibu na Kisiwa cha chumbe Zanzibar.
Meneja Uhusiano wa Mfuko wa
Pencheni { PPF } Bibi Lulu Mengele akiwasilisha salamu za rambi rambi kwa
Makamu wa PILI WA Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kufuatia ajali ya Meli
ya M.V.Skagit iliyotokea wiki iliyopita.
Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akibadilishana mawazo na Bishop Michael wa Kanisa
la Anglikana Dayosisi ya Zanzibar mara baada ya kuwasilisha salamu zao za rambi
rambi hapo ukumbi wa Baraza la wawakilishi Mbweni.
Pembeni ni Katibu Mkuu wa Dayosisi hiyo Bwana Nuhu
Sallanya.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ushirikiano na
Vikosi vya Ulinzi, pamoja na Taasisi za Kiraia imepongezwa kwa hatua iliyochukuwa
katika kukabiliana na Maafa yaliyotokea ya kuzama kwa Meli ya M.V.
Skagit wiki iliyopita.
Pongezi hizo zimetolewa na Uongozi wa Taasisi tofauti
zinazoendelea kutoa mkono wa pole hapa Zanzibar kufuatia vifo vya
watu kadhaa waliokuwemo ndani ya Meli hiyo iliyopata ajali karibu na Kisiwa cha
Chumbe.
Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Pencheni { PPF } Bibi Lulu
Mengele Bishop Michael wa Kanisa la
Anglicana Dayosisi ya Zanzibar pamoja na Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu {
UAE } Bwana Mallallah Mubarak Alameri wakitoa mkono huo wa pole kwa Balozi Seif
walisema hatua hiyo imesaidia kuokoa maisha ya wananchi kadhaa.
Walisema walio wengi wameshuhudia jitihada hizo za
uokozi zilizoleta matumaini ndani ya nyoyo za Jamii.
Hata hivyo wawakilishi hao wa taaasisi tofauti
walisema licha ya juhudi hizo za Serikali lakini bado ipo haja ya msingi ya
kufuatwa kwa sheria na Taratibu sa usafiri wa Baharini.
Walisema utaratibu huo mbali ya kupunguza zinazoweza
kuepukwa lakini pia utasaidia kuondosha mwanya kwa Wafanyabiashara na
Wawekezaji wakorofi wanaoendesha biashara hiyo ya vyombo vya usafiri wa
Baharini.
“ Kitu cha msingi ni kufuatwa kwa sheria na taratibu
za usafiri nah ii itaondosha uzembe na ujanja unaotumiwa na wafanyabiashara
wakorofi”. Alisisitiza Balozi wa UAE Bwana Mallallah.
Naye kwa upande wake Bishop Michael wa Kanisa la
Anglikana la Mkunazini Dayosisi ya Zanzibar
amesema hatua za serikali za kurejesha hali ya amani kufuatia fujo za baadhi ya Vijana zilizofanywa hivi karibuni
imeleta faraja kwa waumini wa kanila lao.
Bishop Michael alisema Uongozi wa Kanisa hilo utaendelea
kuwaelimisha Waumini wao kulinda na kuheshimu amani ya Taifa ambayo inahitajiwa
na kila mwana Jamii.
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi alisema Viongozi wa Serikali wanaendelea kupata matumaini kuona Taasisi na
mshirika mbali mbali ndani na nje ya Nchi yanaunga mkono juhudi za Serikali.
Balozi Seif alisema Serikali kwa upande wake
itaendelea kuchukuwa hatua madhubuti ili kuzuia majanga yanayoweza kuwepukwa
ambayo yamo ndani ya uwezo wa mwanaadamu.
“ Tumeanza kuchukuwa hatua za kukabiliana na hali hii
kwa kuwaomba washirika wetu ndani na nje ya Nchi kutusaidia katika sekta hii Likiwemo
hili zito la upatikanaji wa meli kubwa ya usafirishaji wa wabiria na mizigo”.
Alifafanua Balozi Seif.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
26/7/2012.
No comments:
Post a Comment