Friday, August 31, 2012

SULTAN KING ANG'OA JIKO SEPTEMBA 7

Sultan King bwana harusi mtarajiwa
Hamida Maalim akishow love na bwana harusi mtarajiwa Sultan King
Msanii anaefanya vizuri katika game la muziki wa bongo fleva Zanzibar Sultan King anatarajia kufunga ndoa ijumaa ijayo tarehe 7 mwaka huu na party inatarajiwa kufanyika Salama Hall Bwawani.

BIBI BOMBA NAMBA 3 AREJEA ZANZIBAR, AHOJIWA KATIKA NIPE NIKUPE

Mtangazaji wa kipindi cha Nipe nikupe Husna B
Bi Nasra mshindi wa 3 katika shindano la BIBI BOMBA
Bibi Bomba mshindi wa 3 Bi Nasra akihojiwa na Husna B kwenye kipindi cha Nipe Nikupe  leo akieleza namna shindano lilivyokuwenda mpaka kupatikana mshindi.
Bi Nasra akishow love na Hamida Maalim mara baada ya kumaliza mahojiano yake.

Mzanzibari aliyeshiriki shindano la Bibi Bomba Bi Nasra linalosimamiwa na Clouds TV na Clouds Fm Jijini Dar es Salaam amerejea Zanzibar akiwa amebahatika kuwa mshindi namba 3 na kujinyakulia kiasi cha shilingi milioni moja na nusu taslim (1,500,000/-)

Bi Nasra maarufu kama Bi Naa alieleza changamoto alizokutana nazo kwa kipindi chote walichokuwa katika nyumba maalum waliokuwa wanaishi na kuibatiza jina la Jumba la Dhahabu kutokana na kukamilika kwa mahitaji yote waliyokuwa wakiyahitaji katika nyumba hiyo.
Alisema walikuwa wakishiriki kwenye michezo na mambo mbalimbali waliohitajika kuyafanya ikiwemo kucheza ngoma, mchezo wa kucheza na Nyoka, kupika na kusuka mikeka.

Katika michezo hiyo ipo michezo ambayo aliweza kushiriki ipasavyo na ipo michezo ambayo hakuweza kushiriki kabisa ikiwa ni kucheza ngoma pamoja na kucheza na nyoka.

Bi Nasra anawashukuru wazanzibari wote na watanzania kiujumla kwa kuweza kumpigia kura na kumpelekea kuweza kuwa mshindi namba 3 katika shindano hilo, pia ametoa wito kwa wazanzibari kuweza kushiriki shindano hilo kwa wakati ujao kwani shindano ni zuri na linachangamoto kubwa kwa watu wenye umri kama wake.


Thursday, August 30, 2012

AJALIIIIIIII

WAMACHINGA WANASAIDIA....

Wamachinga wakiwa wamepanga biashara zao pembezone mwa barabara kubwa ya magari maeneo ya kituo bangi (Tanga)
Wamachinga wakiendelea kufanyabiashara zao katika kituo cha daladala Darajani Zanzibar

Inafahamika kwamba hakuna jambo lenye faida bila kukosa hasara, Wafanyabiashara wadowadogo maarufu kama wamachinga ambao mara nyingi biashara zao wanapenda kufanyia pembezone mwa barabara na kwenye vituo vya mabasi wamekuwa ni msaada mkubwa kwa watu kwa kuwarahisishia kupata mahitaji kwa haraka wapitapo barabarani.

Mara nyingi serikali imekuwa ikipiga kelele juu ya wafanyabiashara hao kuwa wawe na sehemu maalum ya kufanyia biashara hizo na kuwatengea maeneo yanayostahili kuwapo. Lakini mbali na kutengewa maeneo wafanyabiashara hao hawapo tayari kuyatumia maeneo hayo wakihofia hawawezi kuwapata wateja wanaowategemea katika biashara zao.

Ni kweli wamachinga ni msaada kwa watu kwa maeneo wanayoyatumia ikiwa ni Stendi za mabasi , vituo vya daladala na pembezoni mwa barabara kwani wanawarahisishia wasafiri kupata mahitaji kwa ukaribu zaidi.

Tatizo kubwa linalopelekea kuwa ni kero kwa watu ni ile hali ya wafanyabishara hao kutumia maeneo ya watembea kwa miguu barabarani kuweka biashara zao hali inayohatarisha maisha ya watembea kwa miguu kwa kukosa sehemu ya kupita na kusababisha wapite barabara kubwa yanapopita magari. Kwa upande wa vituoni wanapelekea msongamano usio kuwa wa lazima na kusababisha hali ya wizi kuongezeka.

Baada ya kuonekana hayo kuna haja ya serikali kuangalia namna nyingine ya kuweza kuwasaidia wafanyabiashara wa namna hii ambao wapo karibia Tanzania nzima.

Tuesday, August 28, 2012

SERIKALI INAHUSIKA HAPO!!


ALI NAHODA MTANGAZAJI WA KIPINDI CHA "RAHA UTAMU" COCONUT FM

Mtangazaji wa kipindi cha Raha Utamu Ali Nahoda

Kama unasikiliza Coconut Fm 88.2 hapo ulipo utakua unapata burudani ya nyimbo za Taarab za taratibu kidogo kupitia kipindi cha Raha Utamu ambacho ndio kipo hewani mda huu. 

Ali Nahoda ndio anatoa vitu vitamu kwelikweli kupitia mawimbi ya Mambo ya Zenji kila siku ya jumatatu hadi ijumaa.

A DAY IS NICE

Show 5 akiwa na Diva Rayshizzle katika Run the Beat
Show 5 Yoram akiwa ametupia ile mbovu
Rayshizzle na Hamida Maalim
Dj dr B na mwanadada Rayshizzle
Hamida Maalim na Dj Dr B
Diva wa Fleva 145 Rayshizzle (Queen of afternoon showz)

Sunday, August 26, 2012

DJ DR B NIMEAMUA KUACHA KAZI COCONUT FM

Dj dr B
Maisha ni safari ndefu sana ambayo mwisho wake ni mwisho wa uhai wako, Pamoja na kuwa maisha ni safari ndefu, hakuna safari inayokosa kituo ni sawa na kwa upande wangu tarehe 30/08/2012 safari yangu ya maisha ya Coconut yanafikia kituo. Nimeamua kuacha kazi kwa sababu zangu binafsi na kupumzika kwa muda nikiwa najipanga kwa mambo yangu mengine..

Najua wengi watatamani kujua sababu nimeamua kufanya hivyo kwaswababu zangu binafsi sina tatizo lolote na ofisi yangu na ninaipenda sana.

Vikwazo na misukosuko ni moja ya njia ya maisha ya mwanadamu tusameheane kwa pale tulipokwenda tofauti na kuangalia maisha mtazamo wa kimaendeleo. Nahitaji ushirikiano wako uendelee kuwapo kama kawaida kwa lolote na popote tuwe pamoja.

 

COCONUT FM,
ZANZIBAR,
                                                                                                                                       01/08/2012     



C.E.O
PRIME TIME PROMOTION
S.L.P
DAR -ES- SALAAM


K.K


MENEJA,
COCONUT FM,
ZANZIBAR.


            YAH: TAARIFA YA KUSITISHA MKATABA

            Tafadhali husika na mada ya hapo juu.

Dhumuni la barua hii ni kuiarifu Kampuni kuwa kutokana na sababu binafsi nimeamua kusitisha mkataba wangu wa kazi kuanzia Agasti 30.2012.

Baada ya kuitumikia Primetime Promotion Ltd kupitia kituo chake cha redio Coconut Fm kwa takribani miaka mitatu na nusu, kwa matakwa yangu binafsi pasipo kushawishiwa na mtu yeyote nimeamua kuacha kazi.

Nashukuru kwa ushirikiano ambao nimepata kutoka kwa uongozi wa Coconut Fm pamoja na Primr time Promotion ,wafanyakazi wenzangu wa Coconut Fm, Prime time Promotion na baadhi ya wafanyakazi wa Clouds Media group kwa kipindi chote ambacho tumekuwa pamoja, nashukuru nimeamua kuondoka kwa amani na ninaamini Kampuni haitosita kunipokea endapo nitahitaji kurudi kufanya kazi na Prime Time Promotion.

Mwisho nawatakia kila la kheri katika harakati za kusukuma mbele gurudumu la maendeleo la Coconut Fm na Prime time Promotions Ltd.

……………………..
Mbaraka Saidi Boha
Program Manager
Coconut Fm 88.2
Mobile No +255 715 982 882
Zanzibar
Tanzania


Saturday, August 25, 2012

"HAIKUWA RAHISI" - SOLID BLACK & MUT LOW

Ramyson Madoro akiwa katika kipindi cha Shusha Fleva
Ramyson Madoro katika Shusha Fleva akizungumza na Solid Black pamija na Mut Low washkaji walioamua kuacha uteja na kuingia kwenye sanaa ya muziki kuielimisha jamii
Solid Black
Mut Low
Kutoka kulia ni Ramyson Madoro,Mut Lowa na Solid Black wakishow love baada ya kumaliza mahojiano kwenye Shusha Fleva.

Haikuwa Rahisi kama ngoma yao inavyoitwa kwa hawa jamaa Solid Black na Mut Lowa kuweza kuachana na hali ya utumiaji wa madawa ya kulevya kwa kipindi cha miaka 7 hali iliyopelekea kupoteza muelekeo wa maisha yao kwa kipindi chote walichokuwa wakitumia madawa ya kulevya.

Black na Mut baada ya kushauriwa kuacha kutumia madawa ya kulevya waliishi Souba house kwa muda wa mwaka mmoja wakiwa na wenzao waliokuwa tayari kuacha kutumia madawa kulevya.
Wameamua kuingia kwenye sanaa ya muziki wa bongo fleva kwa lengo la kuelimisha vijana wenzao kuachana na utumiaji wa mada ya kulevya.

Wimbo wao wa kwanza "Haikuwa Rahisi" walioufanyia studio za T-Top chini ya producer Chief Elia wamechanganya lugha mbili ikiwa ni kiswahili na kiingereza ili kwa yule ambae kiswahili kwake hakipandi ujumbe ataupata kwa lugha ya kiingereza, Solid Black amesimamia vema vesi yake kwa lugha ya kiswahili wakati Mut Low amechana kwa lugha ya kiingereza.

Skiliza ngoma hiyo uone ujasiri wa washkaji kutoka kwenye uteja hadi usanii.....
Solid Black & Mut Low - Haikuwa Rahisi

Friday, August 24, 2012

EXCLUSIVE TRACK "MTOTO WA KARIAKOO" - DULLY SYKES

Dully Sykes - Mtoto wa Kariakoo

ADAM MCHOMVU NA BRAND NEW TRACK AISHA

Listen the brand new track Aisha of Adam Mchomvu

TEN YEARS LATER (Letter to Dandu)

Mambo vp! Jumatatu ya tarehe 27, August, 2012 ni miaka kumi tangu kifo cha marehemu James Maligisa Dandu aka "Mtoto wa Dandu" ama CJ Massive, aliyefariki kwa ajali ya gari jijini Dar es Salaam, August 27, 2002. J apo ni kama vile watu wameanza kumsahau lakini mimi sitoweza kumsahau kamwe. Aliniinspire sana kufanya muziki. So wiki hii mpaka ijumaa nimeamua niitumie kutafakari mazuri aliyoyafanya kwenye muziki wa Tanzania na nimemwandikia barua hii ambayo pia ina wimbo wake hapo kwenye attachment.

Niaje Dandu, Sky hapa tena, nataka kuholla tena
Last time nilikuwa Rock City, your home City
This time nipo Dar city, the Hustles city
August 27, 2002 with a fatal accident, shujaa ukawa umeaga
Ten years later the game is still strong
New Artists, new flows new production
Rap bado ipo ila kiduku ndio fashion
Wanauita muziki wa hela hawaaimbi kwa passion
Muziki yes unalipa vijana wanadrive tu
Gari za maana wachache wamestay true
Show za laki laki humpati huyo Diamond
Humpati AY humpati hata Saigon
Clouds bado wapo watemi kama kawa
Wanapiga tu mahela Fiesta kama dawa
Bongo Records bado ipo ila P-Funk simwelewi
Majani sio Majani, sio Kinywele kimoja tena
Ameshalose focus MJ ye anapeta
Piga sana mkwanja commercial mpaka noma
BSS, matangazo Airtel mpaka Voda
Mchizi yuko safi dread zake safi
Vp maisha ya heaven? Hope it’s all good
Dunia bado mbovu no money no food
Somalia, Eritrea DR Congo
Hakuna maisha bora shida tu hata Bongo
CCM sio shwari this time wanaenda down
CHADEMA wako hot wanaweza chukua hiyo crown
Ufisadi bado upo wa Radar mpaka Dowans
Story zile zile nightmare za Darwin
Siasa na vijana inashika kwa kasi
Sugu ndani ya mjengo alipata nafasi
Zitto, January yule mtoto wa Makamba
Mnyika, Tundu Lissu hawa jamaa wanatamba
Kifupi Tanzania imeshachange sana man
Thanks to the lord bado tunayo amani
Ujinga na maradhi bado tatizo bado lipo
Tumuombe Mungu tuje tuonane tena my brother

Wednesday, August 22, 2012

DJ DR B AM BACK IN UNGUJA

Nimerejea Unguja leo asubuhi na boat ya Kilimanjaro III baada ya kumaliza mapumziko yangu ya mwezi mtukufu wa ramadhani ambayo nimeyamalizia nyumbani kwetu Tanga kunani. I thanks Gog nimefika salama

NILITEMBELEA SHAMBA LETU LILILOPO MICHUNGWANI TANGA

Nikiwa pembeni kidogo ya shamba nikiwaonyesha vibarua mpaka wa kuishia wakati wakilima
Kwa bahati nzuri nilipokuwa nipo nyumbani kwetu Tanga wiki moja baadae baada ya kuwa tayari nimepata nafasi ya kutembelea ndugu na jamaa nilipanga safari ya kwenda kutembelea shamba letu lililopo Michungwani. Furaha kubwa nilikuwa nayo baada ya kufika shambani hapo kwani ni miaka mingi sikuwahi kwenda na mambo mengi nilikuwa nayapata ambayo yalikuwa yakinisikitisha sana, kwa shamba ni hali ya kawaida kusikia mtu analima shamba la mwenzie bila ruhusa na hilo ndilo lilikuwa likilikabili shamba letu.

Nashukuru kwa sasa shamba liko salama na maandalizi ya kilimo cha mwaka huu yameanza kama unavyoona.

Saturday, August 4, 2012

BONYFACE aka HANDSOME BOY AACHIA NGOMA MPYA TOKA “MENSEN SELECTA”

Bonyface a.k.a Handsome Boy

Baada ya kimya cha muda mrefu tangu aachie wimbo wa “ULISEMA” aliomshirikisha Mike T (Mnyalu) ngoma ambayo ilifanya vizuri kwenye vituo mbalimbali vya Redio na TV, Bonyface a.k.a Handsome Boy….Kidume baada ya kuhama mji kasoro bahari Morogoro na kuhamishia ishu zake za muziki Jijini Dar es Salaam ameachia nyimbo mpya matata sana unaoitwa “Bado Mtoto” chini ya producer Mensen Selecta kutoka Studio za STUD DEFFETARTY.

Msanii huo ambae yupo katika Lebo ya Mensen Selecta Deffetarty Music kwa sasa yupo chimbo pamoja na producer wake kupakua mawe mengine ambayo yataachiwa hivi karibuni.

Bonyface a.k.a Kidume ameweka wazi njia za mawasiliano yake ili yeyote mwenye ushauri na maoni kwake aweze kufunguka kupita nambari yake ya simu facebook au email yake kwa lengo la kukuza muziki wa bongo:

Simu  :            0715 600750
Email:-            bonyface.mateza@yahoo.com
Facebook:-    bonyface.mateza@yahoo.com

Friday, August 3, 2012

MTANGAZAJI PEKEE WA VIPINDI VYA TAARAB ZANZIBAR..P LOVER

P. Lover mtangazaji pekee wa kiume wa vipindi vya Taarab

Ni mara chache kusikia vipindi vinavohusu muziki wa Taarab kutangazwa na watangazaji wa kiume kutokana na imani za wanaume wengi kuamini kuwa Taarab ni muziki wa wanawake.

P. Lover mtangazaji wa HITS FM ni mmoja wa watangazaji wa kiume anaewashangaza watu wengi baada ya kuonyesha ubunifu mkubwa wa utangazaji wa kipindi cha Taarab na kuwa na upinzani mkubwa na vipindi kama hivyo vilivyozoeleka kusikika sauti za wanawake, hii ni moja ya ujasiri wa kuonyesha kwamba watu wasiishi maisha ya kukariri kwani kila kitu kinawezekana kwa kila mtu ili mradi kisiwe ni dhambi.

Endapo ingalikuwa muziki wa Taarab ni muziki wa wanawake basi hali hiyo ingalipelekea wanaume wasingaliimba muziki wa aina hiyo, lakini kutokana na kwamba muziki ni kipaji na kipaji hakichagui jinsi kinaweza kuwa kwa mwanaume ama mwanamke na  ndio maana wapo wasanii wengi wa kiume wanaoimba muziki wa aina hiyo.

Mfalme Mzee Yusuf ambae ni mmiliki wa JAHAZI MORDEN TAARAB ni miongoni mwa waimbaji wa kiume wa muziki huo, nani asiye mfahamu Mfalme Mzee Yusuf katika tasnia ya muziki wa Taarab nchini Tanzania na hana mpinzani kutokana na umahiri wake katika utunzi wa mashari mazuri yanayowavutia wanawake na wanaume WHY hajawahi kusita kuimba muziki huo.

Wapo waimbaji wengi wa kike wa muziki wa Taarab kama Malkia Khadija Kopa, Isha Mashauzi na wengine wengi wanaofanya vizuri katika muziki huo. Hali ya upinzani kwa wasanii hawa wakike na Mfalme Mzee Yusuf na waimbaji wengineo wa kiume inafahamika katika jamii ya Tanzania.

Hali hii inadhihirisha kuwa hata kwa upande wa utangazaji pia ni kipaji ambacho anakuwa nacho mtu bila ya kulazimisha wapo wenye uwezo mkubwa wa kutangaza vipindi vinavyohusu muziki wa Hip hop, R & B, Dansi na aina nyinginezo ambao ni wengi kila kona tofauti na upande wa muziki wa Taarab ambako wanaume wengi wanajenga hofu ya kuonyesha vipaji vyao kwa kutangaza vipindi vya muziki huo.

Wednesday, August 1, 2012

RICO SINGLE AJIZUSHIA KUFA KISA KUTAKA UMAARUFU

Rico Sinlge
Imekuwa kawaida kwa wasanii wetu wa muziki Tanzania kujizushia kufa hali inayopelekea kuonyesha udhaifu wa ubunifu katika jamii.

Miaka kadhaa iliyopita ulishawahi kutokea uvumi wa msanii Babu Ayubu kuwa amekufa hali ambayo ilivuma takribani nchi nzima kutokana na umaarufu wake aliokuwa nao kipindi hicho kwa nyimbo zake chache zilizofanya vizuri na kupelekea watu kumfahamu, mbali na uzuri wa nyimbo hizo jamii ilimkubali sana msanii huyo kwa kipaji chake cha kuigiza sauti za viongozi na watu mbalimbali.

Vyombo vya habari vilikuwa kipaumbele katika kuitangaza habari ya kifo cha Babu Ayubu bila kujua kama habari hiyo ilikuwa ni yauzushi. Baada ya muda ilikuja kubainika kuwa msanii huyo aliamua kujizushia yeye mwenyewe habari za kifo chake kwa makusudi wakati taifa tayari lilikuwa linafahamu msanii huyo hayupo tena duniani.

Ayubu aliposakwa na vyombo vya habari baada ya kujulikana hajafa alijitetea kuwa ni habari za uzushi ambazo hajui ni nani aliyezisema.

POLE SANA....DIAMOND

Diamond
Kwa hali isiyotarajiwa Diamond alikuwa katika hali mbaya sana, alikuwa amezidiwa na homa kali ya ghafla iliyosababishwa na kifua kilichomsumbua kwa takribani wiki mbili mfululizo hali iliyopelekea kupelekwa Heameda Medical Clinic kwa Doctor Hery M. Mwandolela, ambaye ni Specialist wa Heart and Cough kwa uchunguzi na vipimo vikubwa kutokana na hali kuwa mbaya.

Baada ya vipimo vyote iligundulika kuwa ni kifua cha kawaida kilisababishwa na tour na ziara nyingi alizozifanya ndani ya mikoa ya Tanzania na nchi mbalimbali kwa mfululizo bila mapumziko.
 
kwa sasa hali ya Diamond si mbaya sana na anawashukuru fans wake wote waliokuwa wakimuombea kupitia Blogs mbalimbali, Twitter, Bbm, Facebook na zinginezo, na Media zote kwa ujumla aweze kupona na kuendelea na shughuli zake za ujenzi wa taifa kama kawaida.