Wednesday, August 1, 2012

RICO SINGLE AJIZUSHIA KUFA KISA KUTAKA UMAARUFU

Rico Sinlge
Imekuwa kawaida kwa wasanii wetu wa muziki Tanzania kujizushia kufa hali inayopelekea kuonyesha udhaifu wa ubunifu katika jamii.

Miaka kadhaa iliyopita ulishawahi kutokea uvumi wa msanii Babu Ayubu kuwa amekufa hali ambayo ilivuma takribani nchi nzima kutokana na umaarufu wake aliokuwa nao kipindi hicho kwa nyimbo zake chache zilizofanya vizuri na kupelekea watu kumfahamu, mbali na uzuri wa nyimbo hizo jamii ilimkubali sana msanii huyo kwa kipaji chake cha kuigiza sauti za viongozi na watu mbalimbali.

Vyombo vya habari vilikuwa kipaumbele katika kuitangaza habari ya kifo cha Babu Ayubu bila kujua kama habari hiyo ilikuwa ni yauzushi. Baada ya muda ilikuja kubainika kuwa msanii huyo aliamua kujizushia yeye mwenyewe habari za kifo chake kwa makusudi wakati taifa tayari lilikuwa linafahamu msanii huyo hayupo tena duniani.

Ayubu aliposakwa na vyombo vya habari baada ya kujulikana hajafa alijitetea kuwa ni habari za uzushi ambazo hajui ni nani aliyezisema.


Habari hiyo hiyo ya kifo cha uongo ikaja kujirejea kwa Mr Blue nae habari za uzushi zilitapakaa kuwa amekufa na kupelekea kushughulisha watu na kuwatia majonzi wale wote waliokuwa wanamfahamu vizuri msanii huyo.

Bado ikaonekana haitoshi miezi michache tu iliyopita msanii wa kike ambaye hayupo chini Tanzania kwa muda mrefu nae alizushiwa habari kama hizo hapa namzungumzia mwanadada Rah P. Kwa bahati nzuri msanii huyu habari zake zilipita kichinichini hali ambayo watu wengi hawakuweza kuisikia.

Kwa mara nyingine tena habari za kifo cha kujizushia zimejirejea usiku wa kuamkia leo ambapo msanii kutoka Zanzibar Rashid Amin Abdallah (Rico Single) ambae ana wiki mbili sasa yupo jijini Dar es Salaam kwa shughuli zake za kimuziki aliamua kujizushia yeye mwenyewe kuwa amekufa.

Habari zilifika Zanzibar majira ya saa 5 usiku kupitia simu yake ya mkononi ambayo alipigiwa Chabi 6 na mtu asiyejulikana na kuambiwa kuwa Rico Single amedondoka ghafla na kuokotwa na wasamaria wema na kumkimbiza hospitali ya Agakhan ambako muda mfupi baadae ilipigwa simu hiyo hiyo na mtu asiyejulikana na kusema Rico Single amefariki dunia baada ya kufika hospitalini hapo.
"Simu yangu ilivyokuwa inaita ilikuwa namba ya Rico Single nilipopokea nikasikia sauti ya mtu ambae simjui akaniuliza mwenye namba hii una mjua nikamwambia ndio si namba ya Rico, akaniambia huyo mwenye simu amedondoka ghafla hivi hapa tunamkimbiza hospitali ya Agakhan hali yake sio nzuri" Chabi 6 alisema hivyo ndivyo alivyoambiwa.
Chabi 6:
"Baada ya muda mfupi nilipigiwa tena kwa namba ile ile ya Rico Single na mtu nisiye mjua akaniambia bwana huyu jamaa tumefika hospitali lakini amesha kufa, mimi nilichikifanya nikaanza kuwapa taarifa wasanii wenzagu haraka kwa sababu nilikuwa sina namba ya ndugu yake yoyote."

Baada ya taarifa hiyo ya kufa kutolewa na mtu asiyejulikana kupitia simu ya msanii huyo hapo hapo simu ilizimwa kitu ambacho kilijaaza hofu kubwa kwa watu kwa sababu hakukuwa na njia nyingine ya haraka ya kuweza kupata habari za uhakika. Hizo zilikuwa habari za awali kufika Zanznibar kuhusu kufariki kwa Rico.

Habari zilipozidi kutapakaa zilizidi kubadilika wapo waliokuwa wakipewa taarifa kuwa msanii huyo kagongwa na gari kakimbizwa hospitali ya Agakhan na wapo waliopewa taarifa ya kuwa alibanwa na Pumu ghafla akafa.

Jitihada kubwa ilifanyika ya wasanii kutoka Zanzibar kuwasiliana na wasanii walipo Dar es Salaam kwa ajili ya kufuatilia habari hizo hospitalini kwa ajili ya kulithibitisha hilo.
Nyumbani kwao:
Wakati hali inaendelea hivyo dada yake alipigiwa simu na kusema hana taarifa yeyeto kuhusu mdogo wake alipokata simu hiyo alipigiwa simu nyingine ambayo ilikuwa ya mama yake mzazi akidondosha kilio kumbe nae alizipata habari za kifo cha Rico Single.

Watu walijaa nyumbani kwa mama yake Rico Single kwa mshtuko mkubwa walioupata baada ya kusikia kilio cha mama huyo, alisikika akilia huku akimtaja mwanae kuwa amemtoka wakati huo ni majira ya saa saba usiku.

Jitihada za wasanii na watangazaji:
Watangazaji wa redio mbalimbali waliendeleza jitihada za kutafuta ukweli huku wakishirikiana na wasanii kwa mawasiliano ya simu, AT ambaye alikuwa mmoja wapo wa kupata taarifa hizo akiwa yupo Dar es Salaam alishirikiana na wenzake kuulizia wapi alipokuwa amefikia msanii huyo, kwa kuwa mara nyingi alipokuwa akiwa Dar alikuwa na wasnii wenzake wa Zanzibar Musa Chombo alijaribu kupiga simu kwenye hotel ambayo waliwahi kufikia pamoja kipindi cha nyuma ambayo inaitwa DAR LIVE HOTEL iliyopo kariakoo.
Musa Chombo " Simu iliita akapokea mhudumu wa mapokezi nikamwambia nahitaji kuongea na Rico Single mhudumu akaniambia huyu hapa ndio anaingia ongea nae akampa simu Rico nikamuita "CHIEF" akakata simu sababu alijua sauti yangu hapo ndio tukaanza kujua kwamba amejisingizia kufa".

Wakati huo AT alikodisha bodaboda saa saba za usiku kutoka Mwananyamalia hadi kariakoo baada ya kuambiwa kwamba Rico alifikia Dar Live Hotel na alijaribu kupiga simu hotelini hapo kabla hajafika na muudumu akamwambia huyo mtu aliondoka tangu saa2 asubuhi hajarudi, AT akamwambia nakuja na polisi hapo ndipo mhudumu huyo akamwambia ukweli kwa yeye aliambiwa na Rico Songle akipigiwa simu awaambie hayupo amepelekwa Agakhan.

Dj Dr B wa Coconut Fm alibahatika kupata namba ya demu wake Rico Single na kumpigia
"Nilimpigia demu wake akasema alikuwa nae mpaka mida ya jioni na baadea akaongea nae na kumwambia amefika salama, nilimwambia achukue taksi aende alipofika sababu alikuwa na jua hadi chumba alichofikia hapo Hotelini na alifanya hivyo kutoka Kinondoni akaenda mpaka hotelini alipofika akanipigia simu akaniambia Rico Single huyu hapa mzima amekaa kwenye makochi anacheka tuu hapa, na maneno yake yalikuwa kama hivi sikiliza hapa.....
"

Ilikuwa ni majira ya saa 8 usiku AT nae alifika hotelini hapo alimkuta amekaa anacheka hali ambayo ilionyesha alikuwa anajua kitu gani kinachoendelea, 
 Msikilize AT alichokisema

Baada ya hapo Rico alimpigia simu mama yake mzazi na kumwambia yeye ni mzima hajui hizo habari zimetoka wapi, wakati huo tayari mama yake amezunguukwa na watu waliokuwa wameenda wakijuwa Rico Single amekufa na mipango ya mazishi ilikuwa tayari imeshapangwa ambapo ilikuwa akazikwe kijijini kwao na mipango ya kusafirisha mwili wake kutoka dar ilikuwa tayari imeshapangwa.

Sikiliza maneno ya Dada yake baada ya kutoka nyumbani kwao ambako walikusanyika watu kwa ajili msiba wa Rico:


Husna B mtangazaji wa kipindi cha Nipe nikupe Coconut Fm alizungumza na Ustaadh ......kuhusiana na swala la mtu anapojizushia kifo katika dini ya Kiislam athari zake ni zipi.
"Mtu anapojizushia kifo kwa ajili ya kuwashughulisha watu au kuhitaji umaarufu ni swala ambalo limekatazwa na linaitwa "Ghushu" au kufanya hadaa na mtu huyo anakuwa sio miongoni mwa waislam na huenda ukajikuta umetolewa na Mtume katika uislam......
Msikilize utaadhi maneno yake:
Ustaadh nae:


Ustaadh anaendelea:


Jambo hili la wasanii kujizushia kufa limekuwa ni mchezo kwa baadhi ya wasanii hapa Tanzania kitu ambacho kinapelekea kuonyesha kuwa wana udhaifu mkubwa katika kazi zao na kuonyesha hali ya kushindwa kumudu kazi ya sanaa hali ambayo inawapelekea kutumia njia ya kujizushia kufa ili mradi jamii iwatambue.

Huu ni ugonjwa kama jamii haikukubali ni bora utafute shughuli nyinge ya kufanya na sio kujizushia kufa.



No comments:

Post a Comment