Msanii Bad Q toka G.A-Unit arachuga
ameachia wimbo wake alomshirikisha Breeze
toka kundi la Machizi flani pamoja na
Ordinary toka Jambo Squad "Huna Hela"
Thursday, July 25, 2013
Bad Q ft Jambo squad & Breeze - Huna Hela
Msanii Chipukizi El Jons aachia ngoma yake mpya "Ukweli wangu"
Anaitwa El Jons, msanii chipukizi anayeishi
Jijini Arusha. ameachia wimbo wake unaoitwa "ukweli wangu"
Washindi wa Tuzo za Wimbo bora wa reggae
Washindi wa Tuzo za Wimbo bora wa reggae
katika Kilimanjaro Music Awards, Warriors
from the East wanakuja na nyimbo mpya "Bongo Reggae" ikiwa ni single yao ya
kwanza kabisa itakayopatikana katika album ya
"Bongo Reggae"
Saturday, July 20, 2013
Miili ya Askari Saba waliofariki huko Darfur yawasili nchini leo
Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi
wa Tanzania (JWTZ) wakipakia moja ya
masanduku saba yenye miili ya askari
wa jeshi hilo waliofariki dunia huko
Darfur nchini Sudan wakati wakilinda
amani, baada ya kuwasili kwenye
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam leo
alasiri.
Miili ya Askari saba wa Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania
(JWTZ) waliofariki Dunia wakati wakiwa
katika kazi ya kulinda amani kwenye Mji
wa Darfur nchini Sudan,imewasili nchini
leo majira ya alasili kwa kutumia ndege
maalumu ya Umoja wa Mataifa.
Askari hao waliuwawa kwa shambulio
la kushtukiza na kundi la waasi wakati
wakiwa kwenye kazi yao ya kulinda
amani nchini Sudan.
Jeshi la JWTZ lilitoa taarifa likisema
kuwa tukio hilo ni pigo kubwa kwa nchi
ya Tanzania ikiwa ni la kwanza kutokea
tangu Tanzania ilipoanza kuchangia
walinzi wa amani chini ya Umoja wa
Mataifa mwaka 2007.
Muddy Kilosa aachia track mpya 'Kosa Langu'
Baada ya kuhamishia shughuli zake za muziki rasmi jijini Dar es salaam kutokea mjini Morogoro Muddy Kilosa ameachia track mpya inayoitwa Kosa Langu.
Msanii huyo ambaye anasimamiwa na meneja wake Mr. Lugano ameachia ngoma hiyo ambayo amerekodi studio za Suductive chini ya producer Mr T Touch na tayari imeanza kuchezwa vituo mbalimbali vya redio.
Ngoma hiyo Imekuwa gumzo kubwa kwa watu kutokana na ustadi wake wa uimbaji na mpangilio mzuri wa mashairi hali iliyompelekea kuzidi kupata mashabiki wengi zaidi na kikubalika katika game la muziki wa Tanzania.
Endapo unahitaji kufanya nae kazi au mahojiano wasiliana nae moja kwa moja kupitia namba yake ya simu ya mkononi 0714 315680.
Endelea kutoa sapoti kwa muziki wa Tanzania.
Wednesday, July 10, 2013
Sajna atoa Official new single "Ningekuwa Single" ft Ben Pol na Sisa Madini
Mkali toka Jijini Mwanza The Rock City SAJNA ameachia official new song aliyomshirikisha BEN POL na SISA MADINI wimbo unaitwa NINGEKUWA SINGLE.
Originally idea ya wimbo huo imetoka kwa Kid boy, na chorus imeandikwa na kid boy pamoja na melody ya chorus.
Verse ya 1 ameandikwa Sajna, Verse 2 ameandika Ben Pol na Verse 3 imeandikwa na Sisa Madini.
Executive producer ni Kid boy, Tetemesha Records DSM.
Vocals za Sajna na Sisa zimefanywa One Love fx Mwanza.
YungEfX ft YungOmega " Day after Day"
YungEfX ft YungOmega wachomoa ngoma mpya ya Day after Day mkono wa noizmekah studios,Pata kusikiliza ngoma HAPA na kwa mawasiliano zaidi check kupitia, www.vmgafrica.com
http://www.hulkshare.com/dl/kdabtghgc9og/Yungefx%20ft%20yungomega-day%20after%20day%20(noiz)?d=1
Endelea kusapoti muziki wa Tanzania.
Vatoloco gangz mixtape coming soon
To all hiphop fans duniani hapa vatoloco gangz wanadrop brand new ngoma inaitwa HIZI FLOW ikiwa ni mixtape project itakayodrop soon kwa mtandao, pata kuskiliza joint hii HAPA ikiwa ni juu ya beat ya mambele, support Tanzania hip hop.
www.vmgafrica.com/
Monday, July 8, 2013
Video game
Ado The Warrior Ft. NuruMuzik & Rich Zion waachia ngoma yao VIDEO GAME ikiwa Beat imetengenezwa na NuruMuzik Vocal Recording / Mixing & Mastering : P-Funk Majani Producer : NuruMuzik & P-Funk Majani Publishing : Bongo Records Limited.
VIDEO GAME NI WIMBO ULIOREKODIWA MWAKA 2012 MWEZI WA 11 NA VIJANA WATATU AMBAO NI : ELINURU NICOLAUS ( NURUMUSIC ) KUTOKA MANYARA miaka 23, DEMETRIUS ADOLPH ( ADO THE WARRIOR ) KUTOKA MBEYA miaka 22, RICHARD ( RICH'ZION ) KUTOKA DAR ES SALAAM miaka 23.
VIJANA HAWA WALIOKUTANA CHUO CHA SANAA BAGAMOYO WAKISOMA KOZI FUPI YA UTAYARISHAJI WA MUZIKI ( MUSIC PRODUCTION ). RICH'ZION KASIMAMA VERSE YA KWANZA NURUMUSIC KASIMAMIA CORAS NA BRIDGE VERSE YA PILI YUPO ADO THE WARRIOR. BEAT LA VIDEO GAME LIMETENGENEZWA NA NURUMUSIC AMBAYE NDIYE ALIYEIMBA CORAS, NA WIMBO HUU UMEREKODIWA NA KUMIXSIWA STUDIO ZA BONGO RECORDS CHINI YA USIMAMIZI WA P.FUNK MAJANI.
Sunday, July 7, 2013
Gsam Original anadrop ngoma Mpya Kabisa "MAMA KUBWA" ,
Gsam Original anadrop ngoma Mpya Kabisa "MAMA KUBWA" , kwaito style track yenye sharp lyrics na dance tempo kwa ajili ya fans wake all over Tanzania na Duniani kote,Ngoma imerekodiwa pande za Noizmekah Production Studios chini ya DefXtro.Pata kisikiliza HAPA na endelea kusupport muziki wa Tanzania,
Saturday, July 6, 2013
Mzigo mpya umefunguliwa leo kwa Zawadi Boha shop barabara ya 13
Nguo za kike za kiume na watoto mzigo mpya
ndio umefunguliwa wahi upatae nguo adimu za
ukweli barabara ya 13 karibu na jengo la
maabara.
Kwa mawasiliano piga 0713700951 au
0767600951.
Wakazi wa Tanga mpango mzima ni sasa.
Monday, July 1, 2013
Magenge brand new track
Brand new Hiphop Track toka kwa Magenge ya
mwenge akiwemo D wa maujanja, K wa
maujanja, Moplus, Gnako pamoja na JcB katika
"Kipande na wana" ikiwa ni mkono toka
Noizmekah, pata kusikiliza HAPA
Saturday, June 29, 2013
Africa kusini waandama kupinga ujio wa Rais Obama
Waandamanaji Nchini Afrika Kusini wakiwa
wamebeba mabango yanayopinga kuja Kwa
Raisi Obama nchini Humo wakati wa
maandamano ya Amani ya Kupinga Kuja Kwa
Obama Katika Jiji la Pretoria Nchini Afrika jana
Jioni - Juni 28
Endelea hapa Jamii forums
Baby J atoa ngoma mpya...Bomoa Bomoa ft Bob Junior.
Mwanadada Jamila Abdalah jina la kwa steji Baby J ameachia wimbo wake mpya unaoitwa Bomoa bomoa akiwa amemshirikisha Bob Junior raisi wa masharobaro. G records ndio imefanyika ngoma hiyo.
Friday, June 28, 2013
Duka la nguo za wajanja barabara ya 13 Tanga
Msimu wa sikuku umefika sasa wajanja wote mnaohitaji kupendeza kwa mitoko ya kisasa, tembelea duka hili lililopo barabara ya 13 mjini Tanga.
Nguo za aina mbalimbali kwa kinadada na kibakaka zinapatikana, viatu, nguo za watoto, madera, top, skin, tait, sketi usiulize utapendezaje nenda ujionee mwenyewe.
Kwa urahisi wa kufika dukani hapo fuata maelekezo haya
Ukitokea Taifa road mtaa wa 13 maarufu mtaa wa maduka ya wachaga unaenda mpaka barabara ya sokoni ngamiani kushoto utaona jengo limeandikwa maabara, utanyoosha kama unaelekea kituo cha daladala za donge upande wa kulia kwako utaona maduka ya simu fuata laini hiyo mpaka utapoona duka la dawa za asili duka linalofuata hapo utakuwa umefika.
Kwa mawasiliano piga 0713 700 951 au 0767 600 951
Nyote mnakaribishwa.
Thursday, June 27, 2013
The Beat Festival
THE BEAT FESTIVAL
Friday 28.06.13
20.00-01.00
Venue: Triniti, Msasani rd. 26, Oysterbay DSM
Entrance: 10.000 tsh only
Lineup:
LUMUMBA- afrofusion
The band also known as Lumumba Theatre, performed at the last edition of Sauti za Busara. The group is made up of talented singers, dancers, actors, choreographers and musicians, based in Dar es Salaam. Established in 1997 by Director Dyuto Komba the group is made up of talented students who have come out of Lumumba Primary School, located in the heart of Dar es Salaam. To date the group has performed all over Tanzania and at festivals in Kenya, Uganda, Mozambique, Germany, Denmark, India and Poland. Lumumba is known for their flamboyant high energy and theatrical performances.
http://www.busaramusic.org/database/artists.php?whereartistid=486
AFRIKWETU- afrofusion
Afrikwetu band, former Afrikali Band, was formed in 2003 and reformed in 2010. The eight bands members all come from different parts of Tanzania and were initially in different bands and decided to to join forces to experience and expand their skills. During their days as Afrikali Band, the group performed at festivals around the world including the US and Europe. Afrikwetu´s experience can be fealt and heard when they perform. In their songs they use different languages from various parts of Tanzanian such as Makonde, Nyakyusa, Nyasa, Nyamwezi and Swahili.
www.afrikwetu.com
MZUNGU KICHAA & ASHIMBA –unplugged
For this edition Mzungu Kichaa will be opening up at THE BEAT with an intimate solo unplugged set featuring the amazing acoustic guitarist Ashimba. Ashimba performed at Mzungu Kichaa´s album launch in Denmark in 2009 and has since released two albums, the second of which has entered the top 20 in the European World Music Charts. Make sure to get to the venue in time to catch this spectacular collaboration (Doors open at 8pm and the first act starts at 9pm)
Dj JD ijumaa hii Isumba Lounge
Sasa tunaamini unafahamu kuwa Night of the
Legends aka usiku wa malegendari isumba
lounge zamani jollies club ndiyo gumzo mjini.
Sasa basi the magic continues, this friday kama
kawaida melegendari tunakutana tunapata
oldies, old scul kali, raga, soca rumba, chacha
na nyingine nyingi. J'mosi hii kama kawaida
moto unaendelea, ma gentleman 50 wataofika
kabla ya saa 6 usiku watapata vol mpya kabisa
The Legend is Back Nonstop cd, wadada 50
kupata a very cold glass of wine mlangoni.
Entry 10k, doors open 9pm. Karibu
Wednesday, June 26, 2013
Angel Classic mdogo wake Vumbe aja na 'Solemba'
Kigoma ni mkoa wenye vipaji vingi vya sanaa hususani katika tasnia hii ya muziki wa kizazi kipya, utapozungumzia wasanii wanaofanya vizuri na kukubalika hapa Tanzania na baadhi ya nchi za jirani basi wengi wao ni kutoka Kigoma.
Vumbe nae akiwa ni miongoni mwa wasanii wazuri kutoka hukohuko Kigoma anathibitisha kuwa kizazi chao kimebarikiwa kipaji cha sanaa hii ya muziki, hapa namzungumzia Angel Classic ambae ameingia kwa kasi na kuachia ngoma yake ya kwanza inayoitwa 'Solemba'
Angel Classic ni mdogo wake Vumbe ambae tayari anafahamika vema katika game, One Time Production ndio ilikofanyika ngoma hii.
Endelea kutoa sapoti ili kuinua vipaji vya hapa nyumbani.
Tuesday, June 25, 2013
Nezzo B ft Lady Yoo "Uko wapi"
Nezzo B anakuja na style ya dance/kwaito katika ngoma yake mpya "Uko wapi" aliyomshirikisha mwanadada Lady yoo.
Na vocal za ngoma hii zimefanyiwa mixing Noizmekah Studio, endelea kusapoti muziki wetu wa Tanzania.
Bofya hapa Pata kusikiliza na download.
www.vmgafrica.com http://www.hulkshare.com/dl/ah4y34b39hxc/Nezzo%20b%20ft%20ladyyoo-uko%20wapi?d=1
Amani aachia ngoma mpya "Haiwezekani"
Anajulikana zaidi kama "Amani" na hapa anakuja na pini jipya "Haiwezekani" ikiwa ni mtindo wa Rap/Hiphop juu ya mdundo wa Defxtro pande za Noizmekah.
Wimbo huu ni mahususi kwa kuwaweka tahadhari watanzania wote na hali ya udanganyifu inayoendelea kisiasa, Ugomvi wa kufikia hatua za kuchafuana majina, vyama vya siasa kuandamana na hata raia wasio na hatia kupoteza maisha katika fujo zinazo sababishwa na siasa.
Amezungumzia pia sekta ya elimu na afya vile vile ufujaji wa pesa za mlipa kodi, Pata wimbo huo hapa "download"
Endelea kutoa sapoti kwa muziki wa Tanzania
Monday, June 24, 2013
ANTI EZEKIEL AJITABIRIA KIFO
WAKATI vifo vikizidi kuwatafuna wasanii, staa
wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel
amefunguka kuwa hawezi kuishi miaka mingi,
atakufa mapema....endelea G5 click
CHILD BENZ ATARAJIA KUMPA SHAVU MWANADADA HABIDA KUTOKA KENYA
Msanii wa muziki wa nchini Tanzania, Chidi
Beenz ama Chuma kama anavyotambulika na
wengi sasa, yupo katika mchongo wa
kufanyakazi ya pamoja na mwanadada Habida
kutoka Kenya, ingawa kwa sasa bado ni
mapema kusema ni kazi gani na itafanyika
wapi? Endelea hapa G5 click
G NAKO AIBUKA NA KANDANDA
G Wara wara toka Crew la Nako2Nako na kampuni ya WEUSI anakuja na SNIPPET yaani KIONJO tu cha wimbo wake mpya utakaoingia sokoni hivi karibuni ikiwa ni mkono toka Noizmekah production studios kwa Defxtro, Snippet hii ni ya wimbo wa " Wara na Mpira http://www.hulkshare.com/rqfljqaby2v4" alomshirikisha Mkali wa RnB BenPol,Sasa hatuelewi Soka na Muziki kwa namna gani vinahusiana hapa ila tumuachie Fanani Gnako atupe ladha kidogo then baadae tutaelewa zaidi, Kwa sasa pata kionjo HAPA na endelea kusupport Muziki wa Tanzania, kwa mawasiliano na mahojiano zaidi check na Gnako mwenyewe kupitia Facebook hapa na kikubwa zaidi ni maboresho ya Muziki na maisha yetu wasanii wa Tanzania, "Kwa mara nyingine nitoe pole kwa familia zote zilizopatwa Misiba ya wasanii wenzetu,Mangwea, Sharo, Langa na nitoe wito kwa wapenzi wa Muziki wa Bongo wasisite kutuunga mkono kwa hali na mali, ningependa kuweka wazi kwa mashabiki wote kuwa wimbo wangu huu "Wara na Mpira" Nitauweka sokoni kwa mauzo kupitia nambari za simu nitakazozitaja hapo baadae ili True fans wangu waweze kuupata wimbo kamili kabla haijasambazwa katika media Yoyote..One love ----http://www.hulkshare.com/rqfljqaby2v4
WATANZANIA AMANI YETU IKO WAPI?
Nchi yetu kwa sasa Inapoteza ule muelekeo wa AWALI tuliokua nao yaani AMANI. Kila kukicha matukio tofauti tofauti ya kuhatarisha AMANI yetu yanatokea kitu ambacho kitatupeleka kwenye VITA vya wenyewe kwa wenyewe.
Mimi kama Rodgers Israel nimeliona hili na kulitazama kwa jicho la tatu ndio maana nimeweza kuwakutanisha wasanii zaidi ya kumi na kuimba wimbo huu wa TUDUMISHE AMANI ili kuikumbusha jamii ya Watanzania na Dunia kwa ujumla kuwa tunapaswa kuilinda AMANI tuliyonayo kwa ajili ya vizazi vijavyo vya nchi yetu.
Ndani ya wimbo huu wameimba wasanii zaidi ya kumi maarufu kama watoto wa Paradise ambao ni Chris wa Jano, Soja B, G wa Simon, G fire, Lady Nike, Mass B, Rayswing The Ngada, Yung Omega, Simpoo, Dj A11, Lady Yoo, Joseph Amani na mimi Rodgers. Wimbo huu umetengenezwa na Producer Soja B kutoka pande za TVC RECORDS Kimandolu Jijini Arusha.
Huo ni ujumbe wa Rodgers ambao ameutuma kupitia mail yangu ukufikie wewe.
Kwa Interviews unaweza kumtafuta kwa +255 764 288 054.
naombeni support yenu ili watu wote wapate huu ujumbe
“WATANZANIA AMANI YETU IKO WAPI, TUKUMBUKE TULIPOTOKA, TULIPO NA TUNAPOKWENDA. MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA IMANI YAKO ITAWALE AMEN.
NACCRI MC "NIONGEZE TENA NYINGINE"
Huyu ni Naccri MC kijana aliyekulia Arusha na kukuzwa kipaji chake ndani ya Tamaduni Music,hii ni singo ya kwanza toka kwenye project yake ambayo anatarajia kuiachia mwishoni mwa mwezi novemba,santuri hiyo itakua na mikwaju 10,na huu ni wa kwanza unaokwenda kwa jina "Niongeze Tena Nyingine" ukiwa umetengenezewa pande za Grandmaster Records na M Lab,msimamizi ni John Blass Sikiliza/Downoad Link: https://soundcloud.com/john-b-jae-grandmaster/niongeze-tena-nyingine-naccri
CHAGA BOY "SIMTAMANI"
ChagaBoy anakuja na ngoma mpya "Simtamani" Toka Nisher Records. Vocal za wimbo huu zimefanywa Noizmekah studios sikiliza HAPA na endelea kuupa shavu muziki wa Tanzania.Powered by www.vmgafrica.com http://www.hulkshare.com/gactz9jye60w
CMPOO - BABY RASTA
Cmpoo mwenye maskani yake Jijini Arusha na
shughuli zake jirani na RocaSigns hapohapo
jijini.
Ameachia ngoma mpya "Baby Rasta' mkono
waDefxtro,Noizmekah Production Studio.
Bofya HAPA kusikilisa na endelea kusapoti
muziki wa Tanzania, Kwa mawasiliano na
mahojiano zaidi check na Cmpoo kupitia +255
757 613 316 powered by www,vmgafrica.com
-------------------------- http://
www.hulkshare.com/o84if41q77k0
Saturday, June 22, 2013
Friday, June 21, 2013
Balozi Seif Iddi amtembelea Sheha aliemwagiwa Tindikali Zanzibar,
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi akimuaga Sheha wa
Shehia ya Tomondo Mohd Omar Said
{ Kidevu } anayekwenda Nchini India kwa
Uchunguzi na Matibabu zaidi baada ya
kumwagiwa Tindi kali usiku wa Tarehe 22
Mei 2013. Sheha Kidevu alikuwa
akipatiwa huduma ya matibabu katika
Hospitali Kuu ya Rufaa Mnazi Mmoja
kwa takriban Mwezi mmoja baada ya
tukio hilo.
Sheha wa Shehia ya Tomondo Moha
Omar Said Kidevu akitoa shukrani kwa
SMZ kwa kufanikisha safari yake ya
kwenda matibabuni Nchini India mbele
ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif ambae hayupo pichani wakati
alipokwenda kumuuga rasmi kwa safari
hiyo. Picha na Hassan Issa wa – OMPR –
ZNZ.
Sheha wa Shehia ya Tomondo Wilaya ya
Magharibi Bwana Mohd Omar Said
{ Maarufu Kidevu } ameondoka Zanzibar
kuelekea Nchini India kwa ajili ya
Uchunguz na matibabu zaidi baada ya
kumwagiwa Tindi kali { Acid } na mtu
asiyejuilikana Usiku wa tarehe 22 Mei
Mwaka huu wa 2013.
Sheha Mohd Kidevu alikuwa akipatiwa
huduma zamatibabu katika Hospitali Kuu
ya Mnazi Mmoja kwa takriban Mwezi
Mmoja sasa kutokana na kuathirika
sehemu ya kulia ya kifua chake, Bega
pamoja na baadhi ya maeneo ya mapaja.
Mgonjwa huyo ameondoka na Ndege ya
shirika la ndege la Oman kwa kupitia
Muscut na amewasili Mjini Chenai Nchini
India mapema leo tarehe 21/6/2013 saa
12.30 za asubuhi akiambatana na Daktari
wake.
Akimuaga sheha huyo hapo katika wadi
yake ya Mapinduzi Kongwe Mnazi Mmoja
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi alimuombea sheha
Mohd Kidevu safari ya mafanikio
itakayomletea hafaja njema.
Bwana Mohd Kidevu alisema Mtu huyo
alianza kutimua mbio baada ya
kufanikiwa kufanya dhambi hiyo kitendo
ambacho akalazimika kuomba msaada
kwa wasamaria wema lakini hatimae
ilishindikana kutokana na kuzidiwa kwa
maumivu makali yenye kuchoma kama
moto.
Sheha huyo wa Shehia yaTomondo
aliendelea kumfahamisha Balozi Seif
kwamba hali yake hivi sasa inaendelea
vyema na ameshaanza
kupatamatumainikufuatiajicho lake
kuanzakuonaingawabadoanakabiliwana
maumivukatikasehemuyakeyausoni.
Naye Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif alimuomba Sheha
huyo wa Tomondo kuwa na moyo wa
subra wakati wa kipindi hichi kigumu
cha huduma za matibabu.
Balozi Seif alimuhakikishia Bwana Mohd
Kidevu kwamba Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar itaendelea kufuatilia matibabu
ya afya yake hadi atakapopata nafuu na
kurejea nyumbani kuendelea na harakati
zake za kimaisha kama kawaida.
Naye sheha wa shehia ya Tomondo Mohd
Omar Said { Kidevu } aliishukuru Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa jitihada
zake zilizosaidia kufanikisha kwa safari
yake ambayo imempa faraja kubwa.
Sheha Kidevu alisema maumivu
yaliyokuwa yakimkabili ndani ya wiki hii
hasa wakati wa kula imepunguwa kidogo
kufuatia huduma za karibu alizokuwa
akipatiwa na madaktari
wanaomuhudumia.
Akizungumza na vyombo vya Habari nje
ya Wodi ya Mapinduzi Kongwe hivi
karibuni wakati alipomkagua sheha huyo
kwa mara ya kwanza Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
alisema Serikali Kuu imesikitishwa na
vitendo hivyo viovu vinavyoleta athari
kwa Binaadamu.
Balozi Seif alisema tabia hiyo mbaya
inayoonekana kuanza kuchipua hapa
Nchini ikibeba ufinyu wa imani inaanza
kuleta hofu miongoni mwa wananchi
katika kuendelea na harakati zao za
kimaisha za kila siku.
Alisema Serikali kupitia vyombo vyake
vya ulinzi itaendelea na uchunguzi wa
kufuatilia matukio hayo na kamwe
haitasita kuwachukulia hatua za kisheria
kwa kuwafikisha katika mkondo wa
sheria wale wote watakaobainika
kuhusika katika vitendo hivyo.
Hili ni tukio la tatu kuwahi kutokea la
kumwagiwa watu tindili kali ndan ya
mkoa wa mjini Magharibi likiwahusisha
aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Baraza la
Manispaa Ndugu Rashid Ali Juma pamoja
na Katibu wa Fufti Mkuu wa Zanzibar
Sheikh Fadhil Suleiman Soraga.
Source michuzi blog
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWEKA JIWE LA MSINGI KWENYE ENEO MAALUM LA UWEKEZAJI MJINI TANGA
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed
Gharib Bilal, akiwahutubia wakazi wa
jijini Tanga, wakati alipofika eneo la
Pongwe jijini Tanga leo Juni 21, 2013 kwa
ajili ya kuweka Jiwe la Msingi la ujenzi
wa Viwanda katika eneo hilo maalum la
Uwekezaji la Tanga Economic Corridor
Sez, linalosimamiwa na Wawekezaji
kutoka nchini Korea Kusini.
MAKAMPUNI YA SIMU KUPANDISHA GHARAMA JULAI MOSI - MOAT
Kufuatia kuongezwa kwa kodi katika
huduma za simu za mkononi , gharama
za huduma hizo zinatajiwa pia
kuongezeka kuanzia Julai Mosi mwaka
huu.
Taarifa ya pamoja iliyotolewa jijini Dar
es salaam na Umoja wa Makampuni ya
Simu za Mkononi Tanzania – MOAT
imesema pendekezo la serikali la kuweka
kodi ya 14.5 kwenye huduma za simu za
mkononi hazotoweza kukwepesha
kupanda kwa gharama za simu kwa
watumiaji.
MOAT inasema awali kodi ilikuwa
ikitozwa asilimia 12.5 katika huduma ya
mawasiliano ya simu na kwmaba
ongezeko la kufiikia asilimia 14.5 tofauti
na nchi za jirani Kenya na Uganda
ambazo zimeendelea kutoza viwango vya
ushuru vya asilimia 10 na 12.5 tu ni
mzigo kwa watumiaji wa huduma za
simu za mkononi.
Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka
2013 unaainisha, huduma za mawasiliano
kuwa ni; “huduma yoyote ya maelezo
inayotolewa na makampuni ya
mawasiliano ya simu kwa njia ya
mawasiliano kwa kutoa au kupokea
sauti, maandishi, na picha au taarifa ya
aina yoyote kupitia mfumo wa
kielektronikia.
”Imesema taarifa hiyo iliyosainiwa na
Vodacom, Airtel, Tigo na Zantel MOAT
imesema eneo mojawapo litakaloathirika
ni huduma za Intaneti eneo amablo
linahitaji kuwekewa mikakati ya kulikuza
kutokana na umuhimu wake katika
maisha ya sasa kiuchumi na kijamii na
wala sio kulizorotesha kwa kusababisha
ongezeko la gharama na hivyo kuendelea
kuwa na kiwango cha cha matumizi
kilinganishwa na baadhi ya nchi nyengine
zikiwemo za Afrika Mashariki. “Hatua hii
ya kuongeza kodi itakwenda kinyume na
mipango iliyopo yenye lengo la kuibadili
jamii kwa kuipatia maarifa ya msingi
kupitia huduma ya intaneti sambamba na
mawasiliano ya simu.”
Kwa mujibu wa MOAT, Tanzania ni kati
ya nchi zenye kiwango cha chini ya
matumizi ya huduma ya mtandao wa
intaneti katika bara la Afrika ambapo
watumiaji wa huduma hiyo ni asilimia 10
pekee ikilinganishwa na nchi jirani ya
Kenya ambayo ina zaidi ya watumiaji
asilimia 40.
Aidha, MOAT imeongeza kuwa,
“mawasiliano ya simu si anasa bali ni
huduma muhimu katika Tanzania ya leo,
sasa tunawezaaje kuwatozakodi mara
kwa mara watu hao hao ambao
wanaitegemea huduma hiyo ili kuboresha
maisha yao? Ilihoji taarifa hiyo ya
MOAT. Taarifa hiyo imeendelea kusema
kuwa kwa tozo la kodi ya mapato ya
asilimia 35 kwenye sekta hiyo ya
mawasiliano ya simu linatosha kiasi ya
kwamba sekta hiyo isngeweza kubeba
mzigo zaidi wa ongezeko jingine.
Hivi sasa, upanuzi wa mawasiliano na
miundombinu vijijini ndiyo kipaumbele
cha sekta nzima. Tunaamini hapa ndipo
ukuaji wa sekta ya mawasiliano ya simu
itakapoonekana katika miaka ijayo.
Ongezeko lolote la kodi litazorotesha
uwezo wetu wa kutanua huduma zetu za
mawasiliano na miundombinu maeneo ya
vijijini, imesema MOAT.
“Tunaelewa kuwa serikali inayafanya
haya yote ili kuweza kupata fedha kwa
ajili ya kusaidia kwenye huduma za jamii
katika maeneo muhimu. Ni bahati mbaya
kwamba sekta ya huduma ya
mawasiliano ya simu inaendelea kubeba
mzigo mkubwa wa ongezeko hili ambapo
wateja watalazimika kuubeba mzigo wa
ongezeko hilo,” ilihitimisha taarifa hiyo
ya MOAT.
NAFASI ZA AJIRA ZA KADA ZA AFYA KWA MWAKA 2012/2013
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
NAFASI ZA AJIRA ZA KADA ZA AFYA
KWA MWAKA 2012/2013
Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi
wa Jamii, anapenda kuwaarifu
Wataalamu wa Kada za Afya kuwa
wamepangiwa vituo vya kazi kutokana
na maombi ya kazi waliyowasilisha
kwake kwa mwaka wa fedha 2012/2013.
Watalamu wote wanatakiwa kuripoti
katika vituo walivyopangiwa kabla ya
tarehe 30 Juni, 2013. Baada ya muda huo
kumalizika waajiri wanatakiwa kutoa
taarifa kwa Katibu Mkuu Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii ili wale ambao
hawajaripoti nafasi zao ziweze kujazwa.
Aidha, Waajiri wote wanakumbushwa
kukagua vyeti halisi (Original) vya
kidato cha nne na kidato cha Sita
pamoja na vyeti vya taaluma kabla ya
kuwaajiri wataalamu hawa wa kada za
afya.
Orodha ya majina ya Wataalamu
waliopangiwa kazi na vituo
walivyopangiwa inapatikana kwenye
tovuti ya Wizara www.moh.go.tz.
Wizara haitatoa barua za kupangiwa
vituo vya kazi kama ilivyokuwa hapo
awali.
Nawapongeza kwa kupata nafasi hii ya
kutumia utaalamu wenu katika
kuwahudumia wananchi, na
ninawatakieni kazi njema na utumishi
uliotukuka.
20 Juni, 2013
Thursday, June 20, 2013
ChopaBoy ft MayChedda
ChopaBoy aka William Munishi ni msanii chipukizi wa rap katika game la muziki wa kizazi kipya anatokea Arusha na hapa ameflow juu ya mdundo wa marekani akimshirikisha mwanadada MayChedda katika chorus ya wimbo HAYA MAISHA pata kuusikiliza HAPA na endelea kusupport muziki wa Tanzania
NEW RELEASE K DOO TOKA WATENGWA FT CHABA
Huyu ni kijana mpya kabisa toka pande za Watengwa ndani ya Arusha, hii ni debute single yake ikiwa kama utambulisho rasmi wa kijana K Doo hapa akiwa ameshirikiana na baba mkubwa Chaba ambaye kwa namna moja ama nyingine amejitolea kwenda bega kwa bega na KDoo katika safari yake ya muziki,ngoma inaitwa Tunakujaza Upepo/Usibonge mkono wa John Blass(John B) toka pande za Grandmaster Records Listen/Download link: www.hulkshare.com/6436yvy7t3sw
John Blass Mallya For, Grandmaster Records, Kaz Studio, Cannibal Shattah & Makini Music +255787276352, +255754201643, +255715201643, +254729990851 www.grandrecs.com www.prezzomusic.com www.kazstudioarusha.blogspot.com
Tuesday, June 18, 2013
P CULTURE FT JCB - LIFE CAN BE
Ni mkono wa Umbwa aka Chindo Man from
Watengwa Family na Vocals zikiwa chini ya
Defxtro wa Noizmekah Productions na Humu
wanapita Sister P-Culture na JCB. Ngoma
inakwenda kwa Jina Life Can Be,ni inspirational
hiphop joint yenye mistari ya kuelimisha jamii,
Pata kuusikiliza HAPA na endelea kusupport
muziki wa Tanzania, kwa mawasiliano zaidi na
Mwanadada P-Culture chek naye kupitia
nambari +255 782 123 700 powered by
www.vmgafrica.com -------------------------
http://www.hulkshare.com/x5o4v6uhaolc
RAFIKI WA MAREHEMU LANGA AELEZA KUHUSU KIFO CHA MSANII HIYO
Na Mwandishi Wetu
MWILI wa mwanamuziki Langa Kileo jana
(Jumatatu) ulipumzishwa kwenye nyumba ya
milele katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar
lakini nyuma ya kifo chake kuna siri ambayo
rafiki yake wa karibu (jina linahifadhiwa) mkazi
wa Mikocheni A jijini Dar ameamua kuiweka
hadharani.
Akizungumza na Uwazi juzi, rafiki huyo wa
marehemu alisema, siku chache kabla ya kifo
chake alimfuata na kumwambia kuwa Israel
mtoa roho anamtembelea usiku na anahisi siku
si nyingi atamfuata mshikaji wake aliyetangulia
mbele ya haki, Albert Mangweha ‘Ngwea’.
“Hii ni siri ambayo hata ndugu zake hawaijui
lakini mshikaji alijua anakufa. Alijitahidi
kukikwepa kifo lakini alishindwa. Siku chache
kabla hajafa, usiku alikuja kwangu na
kuniambia kule kwao kwenye geto lake
analoishi ambalo liko ghorofani, anaona
mauzauza na anahisi kifo kinamuita.
“Nilishangazwa sana na maneno yale. Akazidi
kuniambia eti kwa jinsi mambo yanavyokwenda
hawezi kuendelea kulala kwao na kuanzia siku
ile angelala na mshikaji wetu mwingine pale
Geza, Mikocheni A.
“Kweli siku hiyo alilala pale akiwa na hofu
kubwa na asubuhi baadhi ya watu wakawa
wanamshangaa akiwa ‘amezima’ nje ya lile geto
la mshikaji wake. Alivyoondoka sikumuona tena
mpaka nilipokuja kuambiwa yuko hoi kwa
malaria na kesho yake nikasikia hatunaye,
nimeumia sana,” alisema mtoa habari huyo.
Alipoulizwa juu ya uhusiano wa kifo cha Langa
na matumizi ya madawa ya kulevya, rafiki huyo
alisema: “Inaweza ikawa ngumu kwa ndugu wa
marehemu kuhusisha kifo chake na madawa ya
kulevya lakini mimi namjua Langa nje ndani,
ukweli ni kwamba jamaa alikuwa akiendelea
kula ‘mambo’.
“Alikuwa anakuja maskani tunakula mambo
yetu na hata wakati anafanya kazi kwenye ile
Kampuni ya Barrick hapa Dar, ilikuwa kabla
hajaenda anapita kwanza huku uswahilini kisha
ndiyo anaenda. Kwa maana hiyo malaria ndiyo
iliyomuua lakini hata madawa yamechangia.”
Langa alifariki dunia Juni 13, mwaka huu katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar. Mungu
aiweke roho yake mahali pema peponi. Amini!
SORCE: Globalpublishers
Saturday, June 15, 2013
LADY JAY DEE ATIKISA JIJI KWA SHOW YA MIAKA 13 YA MUZIKI.
Mwanamuziki Lady Jay Dee akiwa kwa steji akionyesha umahiri wa kulishambilia jukwaa
wakati wa show yake ya kutimiza miaka
13 katika Muziki.
Show hiyo iliyofanyika usiku wa
kuamkia leo Nyumbani Lounge,Namanga jijini Dar es Salaam wadau kutoka sehemu mbali
mbali ya Jiji walihudhuria kumpa shavu mwana dada Jide.