Friday, June 21, 2013

MAKAMPUNI YA SIMU KUPANDISHA GHARAMA JULAI MOSI - MOAT

Kufuatia kuongezwa kwa kodi katika
huduma za simu za mkononi , gharama
za huduma hizo zinatajiwa pia
kuongezeka kuanzia Julai Mosi mwaka
huu.
Taarifa ya pamoja iliyotolewa jijini Dar
es salaam na Umoja wa Makampuni ya
Simu za Mkononi Tanzania – MOAT
imesema pendekezo la serikali la kuweka
kodi ya 14.5 kwenye huduma za simu za
mkononi hazotoweza kukwepesha
kupanda kwa gharama za simu kwa
watumiaji.
MOAT inasema awali kodi ilikuwa
ikitozwa asilimia 12.5 katika huduma ya
mawasiliano ya simu na kwmaba
ongezeko la kufiikia asilimia 14.5 tofauti
na nchi za jirani Kenya na Uganda
ambazo zimeendelea kutoza viwango vya
ushuru vya asilimia 10 na 12.5 tu ni
mzigo kwa watumiaji wa huduma za
simu za mkononi.
Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka
2013 unaainisha, huduma za mawasiliano
kuwa ni; “huduma yoyote ya maelezo
inayotolewa na makampuni ya
mawasiliano ya simu kwa njia ya
mawasiliano kwa kutoa au kupokea
sauti, maandishi, na picha au taarifa ya
aina yoyote kupitia mfumo wa
kielektronikia.
”Imesema taarifa hiyo iliyosainiwa na
Vodacom, Airtel, Tigo na Zantel MOAT
imesema eneo mojawapo litakaloathirika
ni huduma za Intaneti eneo amablo
linahitaji kuwekewa mikakati ya kulikuza
kutokana na umuhimu wake katika
maisha ya sasa kiuchumi na kijamii na
wala sio kulizorotesha kwa kusababisha
ongezeko la gharama na hivyo kuendelea
kuwa na kiwango cha cha matumizi
kilinganishwa na baadhi ya nchi nyengine
zikiwemo za Afrika Mashariki. “Hatua hii
ya kuongeza kodi itakwenda kinyume na
mipango iliyopo yenye lengo la kuibadili
jamii kwa kuipatia maarifa ya msingi
kupitia huduma ya intaneti sambamba na
mawasiliano ya simu.”
Kwa mujibu wa MOAT, Tanzania ni kati
ya nchi zenye kiwango cha chini ya
matumizi ya huduma ya mtandao wa
intaneti katika bara la Afrika ambapo
watumiaji wa huduma hiyo ni asilimia 10
pekee ikilinganishwa na nchi jirani ya
Kenya ambayo ina zaidi ya watumiaji
asilimia 40.
Aidha, MOAT imeongeza kuwa,
“mawasiliano ya simu si anasa bali ni
huduma muhimu katika Tanzania ya leo,
sasa tunawezaaje kuwatozakodi mara
kwa mara watu hao hao ambao
wanaitegemea huduma hiyo ili kuboresha
maisha yao? Ilihoji taarifa hiyo ya
MOAT. Taarifa hiyo imeendelea kusema
kuwa kwa tozo la kodi ya mapato ya
asilimia 35 kwenye sekta hiyo ya
mawasiliano ya simu linatosha kiasi ya
kwamba sekta hiyo isngeweza kubeba
mzigo zaidi wa ongezeko jingine.
Hivi sasa, upanuzi wa mawasiliano na
miundombinu vijijini ndiyo kipaumbele
cha sekta nzima. Tunaamini hapa ndipo
ukuaji wa sekta ya mawasiliano ya simu
itakapoonekana katika miaka ijayo.
Ongezeko lolote la kodi litazorotesha
uwezo wetu wa kutanua huduma zetu za
mawasiliano na miundombinu maeneo ya
vijijini, imesema MOAT.
“Tunaelewa kuwa serikali inayafanya
haya yote ili kuweza kupata fedha kwa
ajili ya kusaidia kwenye huduma za jamii
katika maeneo muhimu. Ni bahati mbaya
kwamba sekta ya huduma ya
mawasiliano ya simu inaendelea kubeba
mzigo mkubwa wa ongezeko hili ambapo
wateja watalazimika kuubeba mzigo wa
ongezeko hilo,” ilihitimisha taarifa hiyo
ya MOAT.

No comments:

Post a Comment