Thursday, June 6, 2013

WAKATI TUNAMZIKA MANGWEHA TUWATIBU WENGINEO

KILA nafsi itaonja mauti! Mwenyezi Mungu
ailaze roho ya marehemu Albert Mangwea
‘Ngwea’ mahali pema peponi. Amina.
Ngwea alizaliwa Novemba 16, 1982 na
mauti yamemkuta akiwa katika harakati za
kujikwamua kimaisha. Kabla ndoto zake
hazijatimia, Mungu amempenda zaidi.
Amemchukua. Kazi ya Mola haina makosa,
yatupasa tushukuru kwa yote kama
alivyoimba mkali kutoka Jumba la Vipaji
Tanzania (THT), Lameck Ditto.
Kwenye maisha yake ya kimuziki, Ngwea
alikutana na changamoto kibao likiwemo
suala la ‘menejimenti’ nzuri ya kumsimamia
kazi zake. Ukifanya tathmini ya kina,
mafanikio aliyoyapata kwenye muziki
kamwe huwezi kuyafananisha na jasho
alilovuja kutengeneza jina katika gemu.
Amefanya kazi kubwa, mafanikio yake ni
madogo sana. Hayalingani hata kidogo na
mchango alioutoa kwenye jamii, serikali,
taasisi na makampuni mbalimbali, haitoshi
kumfanya afariki dunia akiwa na mafanikio
kiduchu ya kuishi kwenye geto ambalo bofya G5.com

No comments:

Post a Comment