Na Mwandishi Wetu
MWILI wa mwanamuziki Langa Kileo jana
(Jumatatu) ulipumzishwa kwenye nyumba ya
milele katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar
lakini nyuma ya kifo chake kuna siri ambayo
rafiki yake wa karibu (jina linahifadhiwa) mkazi
wa Mikocheni A jijini Dar ameamua kuiweka
hadharani.
Akizungumza na Uwazi juzi, rafiki huyo wa
marehemu alisema, siku chache kabla ya kifo
chake alimfuata na kumwambia kuwa Israel
mtoa roho anamtembelea usiku na anahisi siku
si nyingi atamfuata mshikaji wake aliyetangulia
mbele ya haki, Albert Mangweha ‘Ngwea’.
“Hii ni siri ambayo hata ndugu zake hawaijui
lakini mshikaji alijua anakufa. Alijitahidi
kukikwepa kifo lakini alishindwa. Siku chache
kabla hajafa, usiku alikuja kwangu na
kuniambia kule kwao kwenye geto lake
analoishi ambalo liko ghorofani, anaona
mauzauza na anahisi kifo kinamuita.
“Nilishangazwa sana na maneno yale. Akazidi
kuniambia eti kwa jinsi mambo yanavyokwenda
hawezi kuendelea kulala kwao na kuanzia siku
ile angelala na mshikaji wetu mwingine pale
Geza, Mikocheni A.
“Kweli siku hiyo alilala pale akiwa na hofu
kubwa na asubuhi baadhi ya watu wakawa
wanamshangaa akiwa ‘amezima’ nje ya lile geto
la mshikaji wake. Alivyoondoka sikumuona tena
mpaka nilipokuja kuambiwa yuko hoi kwa
malaria na kesho yake nikasikia hatunaye,
nimeumia sana,” alisema mtoa habari huyo.
Alipoulizwa juu ya uhusiano wa kifo cha Langa
na matumizi ya madawa ya kulevya, rafiki huyo
alisema: “Inaweza ikawa ngumu kwa ndugu wa
marehemu kuhusisha kifo chake na madawa ya
kulevya lakini mimi namjua Langa nje ndani,
ukweli ni kwamba jamaa alikuwa akiendelea
kula ‘mambo’.
“Alikuwa anakuja maskani tunakula mambo
yetu na hata wakati anafanya kazi kwenye ile
Kampuni ya Barrick hapa Dar, ilikuwa kabla
hajaenda anapita kwanza huku uswahilini kisha
ndiyo anaenda. Kwa maana hiyo malaria ndiyo
iliyomuua lakini hata madawa yamechangia.”
Langa alifariki dunia Juni 13, mwaka huu katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar. Mungu
aiweke roho yake mahali pema peponi. Amini!
SORCE: Globalpublishers
Tuesday, June 18, 2013
RAFIKI WA MAREHEMU LANGA AELEZA KUHUSU KIFO CHA MSANII HIYO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment