Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi akimuaga Sheha wa
Shehia ya Tomondo Mohd Omar Said
{ Kidevu } anayekwenda Nchini India kwa
Uchunguzi na Matibabu zaidi baada ya
kumwagiwa Tindi kali usiku wa Tarehe 22
Mei 2013. Sheha Kidevu alikuwa
akipatiwa huduma ya matibabu katika
Hospitali Kuu ya Rufaa Mnazi Mmoja
kwa takriban Mwezi mmoja baada ya
tukio hilo.
Sheha wa Shehia ya Tomondo Moha
Omar Said Kidevu akitoa shukrani kwa
SMZ kwa kufanikisha safari yake ya
kwenda matibabuni Nchini India mbele
ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif ambae hayupo pichani wakati
alipokwenda kumuuga rasmi kwa safari
hiyo. Picha na Hassan Issa wa – OMPR –
ZNZ.
Sheha wa Shehia ya Tomondo Wilaya ya
Magharibi Bwana Mohd Omar Said
{ Maarufu Kidevu } ameondoka Zanzibar
kuelekea Nchini India kwa ajili ya
Uchunguz na matibabu zaidi baada ya
kumwagiwa Tindi kali { Acid } na mtu
asiyejuilikana Usiku wa tarehe 22 Mei
Mwaka huu wa 2013.
Sheha Mohd Kidevu alikuwa akipatiwa
huduma zamatibabu katika Hospitali Kuu
ya Mnazi Mmoja kwa takriban Mwezi
Mmoja sasa kutokana na kuathirika
sehemu ya kulia ya kifua chake, Bega
pamoja na baadhi ya maeneo ya mapaja.
Mgonjwa huyo ameondoka na Ndege ya
shirika la ndege la Oman kwa kupitia
Muscut na amewasili Mjini Chenai Nchini
India mapema leo tarehe 21/6/2013 saa
12.30 za asubuhi akiambatana na Daktari
wake.
Akimuaga sheha huyo hapo katika wadi
yake ya Mapinduzi Kongwe Mnazi Mmoja
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi alimuombea sheha
Mohd Kidevu safari ya mafanikio
itakayomletea hafaja njema.
Bwana Mohd Kidevu alisema Mtu huyo
alianza kutimua mbio baada ya
kufanikiwa kufanya dhambi hiyo kitendo
ambacho akalazimika kuomba msaada
kwa wasamaria wema lakini hatimae
ilishindikana kutokana na kuzidiwa kwa
maumivu makali yenye kuchoma kama
moto.
Sheha huyo wa Shehia yaTomondo
aliendelea kumfahamisha Balozi Seif
kwamba hali yake hivi sasa inaendelea
vyema na ameshaanza
kupatamatumainikufuatiajicho lake
kuanzakuonaingawabadoanakabiliwana
maumivukatikasehemuyakeyausoni.
Naye Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif alimuomba Sheha
huyo wa Tomondo kuwa na moyo wa
subra wakati wa kipindi hichi kigumu
cha huduma za matibabu.
Balozi Seif alimuhakikishia Bwana Mohd
Kidevu kwamba Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar itaendelea kufuatilia matibabu
ya afya yake hadi atakapopata nafuu na
kurejea nyumbani kuendelea na harakati
zake za kimaisha kama kawaida.
Naye sheha wa shehia ya Tomondo Mohd
Omar Said { Kidevu } aliishukuru Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa jitihada
zake zilizosaidia kufanikisha kwa safari
yake ambayo imempa faraja kubwa.
Sheha Kidevu alisema maumivu
yaliyokuwa yakimkabili ndani ya wiki hii
hasa wakati wa kula imepunguwa kidogo
kufuatia huduma za karibu alizokuwa
akipatiwa na madaktari
wanaomuhudumia.
Akizungumza na vyombo vya Habari nje
ya Wodi ya Mapinduzi Kongwe hivi
karibuni wakati alipomkagua sheha huyo
kwa mara ya kwanza Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
alisema Serikali Kuu imesikitishwa na
vitendo hivyo viovu vinavyoleta athari
kwa Binaadamu.
Balozi Seif alisema tabia hiyo mbaya
inayoonekana kuanza kuchipua hapa
Nchini ikibeba ufinyu wa imani inaanza
kuleta hofu miongoni mwa wananchi
katika kuendelea na harakati zao za
kimaisha za kila siku.
Alisema Serikali kupitia vyombo vyake
vya ulinzi itaendelea na uchunguzi wa
kufuatilia matukio hayo na kamwe
haitasita kuwachukulia hatua za kisheria
kwa kuwafikisha katika mkondo wa
sheria wale wote watakaobainika
kuhusika katika vitendo hivyo.
Hili ni tukio la tatu kuwahi kutokea la
kumwagiwa watu tindili kali ndan ya
mkoa wa mjini Magharibi likiwahusisha
aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Baraza la
Manispaa Ndugu Rashid Ali Juma pamoja
na Katibu wa Fufti Mkuu wa Zanzibar
Sheikh Fadhil Suleiman Soraga.
Source michuzi blog
No comments:
Post a Comment